Wamarekani waanza kurejea katika maisha yao. | Masuala ya Jamii | DW | 31.10.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Wamarekani waanza kurejea katika maisha yao.

Mamilioni ya watu waliokumbwa na baa kubwa la kimbunga Sandy huko katika maeneo ya kaskazini/mashariki mwa Marekani leo hii watajaribu kurejesha hali yao ya maisha ya kawaida inagawa bado kuna changamoto kadhaa.

Aerial views shows the damage caused by Hurricane Sandy to the New Jersey coast taken during a search and rescue mission by 1-150 Assault Helicopter Battalion, New Jersey Army National Guard on October 30, 2012. REUTERS/Mark C. Olsen/U.S. Air Force/Handout (UNITED STATES - Tags: DISASTER ENVIRONMENT TPX IMAGES OF THE DAY) FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. IT IS DISTRIBUTED, EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS

Kimbunga Sandy

Kimbunga Sandy kimeathiri usafiri wa umma pamoja na mfumo wa nishati umeme kwa kiasi kikubwa katika maeneo kadhaa ya jiji la New York na itachukua siku kadhaa pia kurejeshwa kwake katika hali ya kawaida. Ikiwa ni siku sita kabla ya uchaguzi wa rais wa Marekani, yaani Novemba 6, Rais Barack Obama atatembelea eneo ambalo limevurugwa kabisa na kimbunga hicho la ufukwe wa New Jersey.

Katika ziara yake hiyo ataongozwa na Gavana wa eneo hilo ambae anatoka chama cha Republican Chris Christie ambae anamuunga mkono mpinzani wake Mitt Romney ambae hata hivyo amemsifu Obama na Juhudi za serikali katika kukabiliana na kimbunga hicho.

Mazingira magumu kwa Romney

Mitt Romney, former Republican presidential candidate and governor of Massachussetts, speaks at the Republican National Convention 2008 at the Xcel Energy Center in St. Paul, Minnesota, on September 03, 2008. AFP PHOTO Paul J. RICHARDS (Photo credit should read PAUL J. RICHARDS/AFP/Getty Images)

Mgombea urais Mitt Romney

Kadhia hii imemuweka katika mazingira magumu ya kisiasa Romney ambae mwaka uliyopita alinukuliwa akisema shirika la serikali la kukabiliana na majanga ya dharura lifungwe na majukumu yake yaachwe kwa majimbo husika. Na sasa imebakia wiki kabla ya uchaguzi ukiwa unakwenda sawia na janga hilo kubwa la kimbunga. Kampeni ya Romney inawahikishia wapiga kura kwamba utawala wake utahakikisha waathiriwa wa majanga hawateseki.

Viongozi katika ngazi zote wana kazi kubwa sana kurejesha katika hali ya kawaida maeneo yenye wakazi wengi yalikuwa katika pwani ya Mashariki nchini Marekani.

Kimbunga Sandy kinakadiriwa kugharimu maisha ya watu wa 40 nchini humo,na kupiga kutoka kutoka upande wa majini na kutpa theluji katika milima ya Milima ya Apalachian, zaidi ya makazi ya watu milioni 8.2 sambamba na maeneo ya biashara yalibaki pasipo umeme katika majimbo kadhaa.

Hali mbaya New York

FILE - In this Feb. 3, 2010 file photo, a sand hog works inside the massive cavern for the new 34th Street Station in New York that was carved out by giant tunnel boring machines. On Monday, July 23, 2012 the last of the 200-ton tunnel boring machines finished its mission digging 13 miles of new train tubes deep beneath New York City. The seven machine fleet bored through bedrock and created 16 new tunnels in 4 ½ years of digging. (Foto:Mary Altaffer, File/AP/dapd)

Njia ya Treni

Njia za reli na barabara ambazo zinatumiwa na idadi kubwa sana ya watu jijini New York zilijaa maji. Nusu ya eneo la Manhattan limeendelea kutokuwa na umeme baada ya kutokea mripuko katika kituo kidogo cha umeme kinachohudumia eneo hilo Con Edison.

Kimbunga hicho kilisukuma maji katika jiji la New York kwa urefu wa futi 14 na kwamba kutokana na hilo jiji hilo, serikali inasema wakazi wake wataendelea kutabika pasipo kutumia njia za chini zenye umuhimu mkubwa kwa siku kadhaa.

Usafiri wa mabasi una mipaka yake kwa hivyo watu wengi wanatembea umbali mrefu kwa miguu au kutumia taxi katika mitaa ya jiji hilo.

Mwandishi: Sudi Mnette/AFP/APE
Mhariri:Yusuf Saumu

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com