1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walioambukizwa COVID-19 wafikia zaidi ya laki tatu duniani

Sekione Kitojo
22 Machi 2020

Karibu watu bilioni moja duniani kote wamelazimika kubakia majumbani mwao leo Jumapili(22.03.2020), vifo vya Corona vikifikia watu 13,000 na viwanda vimefungwa nchini Italia baada ya idadi ya vifo kuwa juu kwa siku moja.

https://p.dw.com/p/3Zs17
Coronavirus in Indien Ausgangssperre
Picha: AFP/I. Mukherjee

Janga hili la virusi vya corona limelazimisha  mataifa 35 kuwataka wananchi  wao wasitoke ovyo  nje, na kusababusha  kuvurugika kwa hali  ya  maisha, usafiri  na  biashara wakati  serikali  zikijaribu kufunga  mipaka na  kutoa  mamia  kwa mabilioni  ya  dola  kama hatua ya  dharura  ya  kuepuka  athari ya kuharibika  kabisa  kwa uchumi kwa kiwango kikubwa.

New York: Auswirkungen des Coronavirus auf die US-Aktienmärkte
masoko ya fedha yameporomoka kwa kiasi kikubwa kutokana na janga la virusi vya coronaPicha: picture-alliance/dpa/M. Nagle

Zaidi ya  maambukizi 300,000 yamethibitishwa  duniani  kote, ambapo  hali  inaendele  kuwa  mbaya nchini  Italia ambako  idadi ya vifo imepanda  hadi  zaidi  ya  watu 4,800, ikiwa  ni  zaidi  ya  theluthi ya  jumla  ya  vifo  vyote duniani.

Waziri  mkuu Gouseppe Conte  alitangaza  kufungwa  kwa viwanda ambavyo havizalishi  bidhaa  za  lazima  katika  hotuba  aliyotoa kupitia  televisheni  jana  Jumamosi,(21.03.2020).

Taifa  hilo  la  eneo  la  Mediterania  lenye  wakaazi  wapatao milioni 60  hivi  sasa  ni  kitovu  cha  ugonjwa  huo , ambao  kwanza ulijitokeza katikati ya  China mwaka  jana  kabla  ya  kutoka  nje  ya mipaka  ya  nchi  hiyo  na  kusambaa  duniani  kote.

Italia  hivi  sasa  imeripoti  vifo  zaidi  kuliko  China  bara na  nchi  ya tatu Iran  kwa  pamoja, na  ina  kiwango  cha  vifo  cha  asilimia  8.6 miongoni mwa  maambukizi  yaliyothibitishwa  ya  COVID-19, ikiwa ni kiwango  cha  juu  kuliko  karibu  nchi  nyingine.

Nchini  Marekani , zaidi  ya  theluthi  moja  ya  Wamarekani wanajaribu  kubadili  maisha   katika  awamu  mbali  mbali  za kufungiwa  ndani, ikiwa  ni  pamoja  na  miji  ya  New York , Chicago na  Los Angeles. Maeneo  mengine  ya  Marekani  yanatarajia kuongeza  vizuwizi pia.

USA Vizepräsident Mike Pence
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence akitoa maelezo kuhusu janga la virusi vya CoronaPicha: picture-alliance/CNP/AdMedia/A. Drago

"Huu ni  wakati wa kujitolea  muhanga kwa  pamoja, lakini  pia  ni muda  wa  kuthamini wapendwa  wetu," Rais wa  Marekani  Donald Trump  amesema. "Tutapata ushindi  mkubwa."

Dunia yapambana na  virusi vya corona

Wakati  viongozi  wa  dunia  wameapa  kupambana  na  janga  hili, idadi ya  vifo  na  maambukizi  vimeendelea  kuongezeka , hususan barani  Ulaya,  kwa  hivi  sasa  ikiwa  ndio sehemu  hatari  ya ugonjwa  huo wa virusi  vya  Corona.

Uhispania imeripoti ongezeko  la  asimilia 32 katika  vifo  vipya  jana Jumamosi, ambapo  waziri  mkuu  Pedro Sanchez ameonya  kuwa taifa  hilo  linahitaji kujitayarisha  kwa  kile  alichosema "siku zenye matatizo makubwa  huko  mbeleni".

Italien - Turin -Coronavirus
Msururu wa watu wakisubiri kununua mahitaji katika duka la vyakula mjini Turin , nchini Italia..Picha: picture-alliance/AP/M. Alpozzi

Vifo  nchini  Ufaransa  vimefikia  watu 562 wakati  maafisa  wa  polisi wakisema  helikopta na  ndege zisizokuwa  na  rubani  zimewekwa kuimarisha  juhudi  za  serikali  kuona  kwamba  watu  wanabakia majumbani  mwao.

janga  hili limevuruga  masoko ya fedha  ya  dunia, na  Marekani , ambayo  ina  uchumi  mkubwa  duniani , inajitayarisha  kuingiza katika  uchumi fedha  nyingi  za  kuchochea  uchumi  ambazo zinaweza  kufikia  dola  trilioni 1.  Mamilioni wametakiwa  kubakia nyumbani  nchini Marekani.

Wakati huo huo kiongozi mkuu  wa  Iran  Ayatollah Ali Khamenei amekataa  msaada  wa  Marekani  leo  kupambana  na  virusi  vya corona, akielezea  dhana ya njama  ambazo  hazieleweki  kuwa virusi hivyo  inawezekana  kuwa  vimetengenezwa  na  binadamu kutokea  Marekani.

Iran Teheran Rede Khamenei
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei akihutubia taifa mjini TeheranPicha: picture-alliance/AP/Office of Iranian Supreme Leader

Matamshi  hayo  ya  Ayatollah Ali Khamenei  yanakuja  wakati  Iran inakabiliwa  na  vikwazo  vikali vya  Marekani  vikizuwia  nchi  hiyo kuuza  mafuta yake  ghafi na  kuweza  kutumia masoko ya  kimataifa. Lakini  wakati  maafisa  wa  Iran  katika  siku  ya  hivi  karibuni wamekosoa  vikwazo  hivyo, Khamenei  badala  yake  ameamua kuleta   dhana hiyo  ya  njama  ambayo  imekuwa  ikitumiwa  na maafisa  wa  China juu  ya  virusi  hivyo  vipya  katika  hatua  ya kukwepa  lawama  kutokana  na  janga  hilo.