Walibya waadhimisha vuguvugu la mapinduzi | Matukio ya Kisiasa | DW | 16.02.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Walibya waadhimisha vuguvugu la mapinduzi

Maelfu ya watu walikusanyika katika miji miwili mikubwa nchini Libya,yaTripoli na Benghazi Ijumaa(15.02.2013)kusherehekea miaka miwili tangu kuanza kwa mapinduzi yaliyosababisha kuangushwa kwa Moammar Gaddafi.

TRIPOLI, Feb. 15, 2013 (Xinhua) -- Libyans attend a celebration for the second anniversary of the unrest that toppled former leader Muammar Gaddafi, in Martyrs' Square in the Libyan capital Tripoli, Feb. 15, 2013 (Xinhua/Hamza Turkia) XINHUA /LANDOV Keine Weitergabe an Drittverwerter.

Maadhimisho ya mwaka wa pili wa kuondolewa utawala waGaddafi mjini Tripoli

Katikati ya jiji la Tripoli, mamia yawatu walikusanyika katika uwanja wa mashahidi , wakipepea bendera na maputo na kuimba nyimbo za kusifu mashahidi waliokufa katika mapinduzi ya Libya wakati magari yakipita mjini wakipiga honi.

Mjini Benghazi, mji wa mashariki ambako ulianzia uasi , maelfu yawatu waliandamana katika njia ile ileya maandamano yaliyofanyika Februari 15 , mwaka 2012, kichocheo ambacho kilizusha vuguvugu la mapinduzi siku mbili baadaye.

Protesters from Bani Walid demonstrate outside Libya's national congress compound in Tripoli October 21, 2012. About 500 protesters broke into the grounds of Libya's parliament building on Sunday to demand an end to violence in Bani Walid, a former stronghold of Muammar Gaddafi that is being shelled by militiamen from a rival town. REUTERS/Ismail Zitouny (LIBYA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST) // eingestellt von se

Maandamano mjini Tripoli

Waandamanaji Benghazi

Waandamanaji wa Benghazi pia waliwasifu mashahidi , pamoja na wale ambao wamepotea na wale ambao wamejeruhiwa katika mzozo ambao ulidumu kwa zaidi ya miezi minane hadi pale alipouwawa kanali Gaddafi Oktoba 20, mwaka 2011. Lakini waandamanaji pia wamekosoa viongozi wapya, wakidai hususan kugawana zaidi madaraka.

Serikali tayari imechukua hatua madhubuti za kudhibiti jaribio lolote la waungaji mkono wa utawala wazamani kufanya fujo huku waandamanaji wakiwa na hasira wanawashutumu watawala wapya kwa kushindwa kuleta mabadiliko.

Baadhi yawakosoaji wa serikali wamediriki hata kutoa wito wa mapinduzi mapya, wakati wakishutumu madaraka ya wanamgambo wa zamani ambao walisaidia kufikisha mwisho utawala wa kanali Gaddafi wa zaidi ya miongo minne.

People celebrate Libya's liberation in Misrata on Oct. 23, 2011, after the death of former leader Muammar Gaddafi. Gaddafi's body was temporarily displayed in the western Libyan city.

Sherehe mjini Tripoli kusherehekea miaka miwili tangu kuondolewa utawala waGaddafi

Maandamano yafutwa

Wakati huo huo viongozi wa makundi yanayotaka kupata utawala wa ndani waeneo la mashariki ya Libya wamefuta maandamano yaliyopangwa kutokana na hofu za kutokea ghasia jana ijumaa, wakati maelfu yawatu waliingia mitaani kuadhimisha miaka miwili tangu kuanza kwa vuguvugu la mapinduzi nchini humo.

Makundi mjini Benghazi, yanayojita , vuguvugu la mapinduzi ya mwaka 2011 ambayo yalimuondoa kanali Gaddafi kutoka madarakani, yalitayarisha maandamano makubwa kudai usalama zaidi na uwekezaji katika mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Libya.

SIRTE, LIBYAN ARAB JAMAHIRIYA: A delegate walking in a hallway of the Sirte Conference Centre observes a billboard with Libyan president Muammar Khadafi hosting the Fifth Ordinary Session of the Assembly of the African Union 03 July 2005. Preliminary and comity meetings are being held in this city 450 kilometers east of Tripoli in preparation to the two-day presidential summit expected 04 July. AFP PHOTO/CRIS BOURONCLE (Photo credit should read CRIS BOURONCLE/AFP/Getty Images)

Bango linalomwonesha dikteta Gaddafi

Hali ilikuwa ya mchanganyiko baina yawale waliokuwa wakiimba kwa furaha na kupunga bendera na wale waliokuwa wakiimba wimbo wa taifa, nyuso zao zilipakwarangi ya bendera ya Libya, na wale ambao walikuwa wamesimama tu wakutumbua macho bila kuonyesha hisia yoyote.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre /afpe

Mhariri: Sudi Mnette

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com