1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walia wakiondolewa katika eneo la waasi nchini Syria

Sekione Kitojo
25 Machi 2018

Wasyria walipanda mabasi huku machozi yakiwatiririka Jumapili wakati wakiondoka kutoka eneo ya Ghouta mashariki lililoharibiwa kwa  vita, katika wimbi la kuwaondoa watu kutoka eneo ambalo ni ngome ya zamani wa waasi.

https://p.dw.com/p/2uwgY
Syrien Ost-Ghouta
Picha: picture-alliance/dpa/Sana

Wiki tano  tangu  utawala  wa  Syria  kuanzisha mashambulizi  makali dhidi  ya  Ghouta , sasa inashikilia  zaidi  ya  asilimia  90 ya eneo  hilo  ambalo lilikuwa  ngome  kuu  ya upinzani  nje kidogo  ya  mji  mkuun  Damascus.

Syrien Ost-Ghouta
Raia pamoja na wapiganaji wakiondoka kutoka Ghouta masharikiPicha: picture-alliance/dpa/Sana

Kuusaidia  utawala  wa  Syria  kukamata eneo  lote, muungano  mkono  mkubwa  wa  serikali hiyo Urusi imefanya  mazungumzo  ya  upatanishi na  makundi  mbali  mbali  ya  waasi kujadili  kuhusu  kuondoka  kutoka  katika  maeneo matatu yaliyobaki.

Moja  kati  ya  eneo  hilo liliondolewa  watu  chini  ya  makubaliano  hayo  katika  siku  za  hivi karibuni na  uondoaji  wa  watu ulianza baadaye  siku  jana  Jumamosi(24.03.2018) kwa sehemu  ya  pili, inayoshikiliwa na  kundi  la waasi wenye  itikadi  kali  ya  Kiislamu  la Faylaq al-Rahman.

Makubaliano  hayo  yanapagwa  kushuhudia  kiasi  ya  waasi 7,000 na  raia walichukuliwa kwa  mabasi  kutoka  miji ya  Arbin na  Zamalka  na  katika  wilaya  ya  Jobar kwenda  katika jimbo  linalodhibitiwa  na  waasi  la  Idlib  kaskazini  magharibi  mwa  Syria.

Baada  ya  uchelewesho  wa  masaa  kadhaa , kiasi  ya  raia 980 waliondolewa  kutoka Ghouta  usiku  wa  Jumamosi kwa  mabasi  yapatayo 17  pamoja  na  magari kadhaa  ya kubebea  wagonjwa.

Syrien Krieg - Ostghuta bei Damaskus | Evakuierung aus Harasta, Ostghuta
Mlolongo wa mabasi ukisubiri kuwachukua watu kutoka Ghouta masharikiPicha: Reuters/O. Sanadiki

Waliwasili  katika  sehemu  ya  jimbo  la  Hama  karibu  na  mpaka  na Idlib asubuhi  ya Jumapili.  Hatua  mpya  ya  kuwaondoa  watu  inatarajiwa  kufanyika  leo Jumapili (25.03.2018).

Wabeba vitu vichache

Raia  wa  Syria  waliofadhaika  pamoja  na  wapiganaji  wa  makundi  ya  waasi  wakivalia mavazi  meusi  walijikusanya  majira  ya  asubuhi katika  mitaa mikuu ya  Arbin , mwandishi wa  shirika  la  habari  la  AFP katika  eneo  hilo  alisema.

Walimebeba  mifuko mikubwa  na  kuburura  masanduku  yaliyojaa hadi  pomoni  wakati wakipita  katika  majengo  yaliyoharibiwa. Ilipofika asubuhi , kiasi  ya  mabasi 20 yaliyokuwa tupu  na  magari  ya  kubebea  wagonjwa  yalikingia katika  mji huo, yakiegeshwa  katika eneo  kubwa  la  makutano  ya  barabara.

Wapiganaji  na  raia  walianza  kuingia  katika  mabasi  hayo, wakiaga  nyumba  zao  huku machozi  yakiwatiririka  kabla  ya  kusafiri kuelekea  katika  eneo  la  wapinzani  upande  wa kaskazini.

Syrien Ost Ghouta Zerstörung Opfer
Mji wa Douma katika Ghouta mashariki ulivyoharibiwaPicha: picture-alliance/AA/M. Abu Taim

Hamza Abbas , mwanaharakati  wa  upinzani  katika  mji  wa  karibu  wa  Zamalka, aliliambia shirika  la  habari  la  AFP  anapanga  kupanda  pia  basi  na  kuondoka.

"Watu  wana huzuni  sana  kwa  kuondoka  kwenye  nyumba  zao, ardhi  yao , kumbukumbu ya  utoto  wao na  sehemu  ambayo  waliishi katika  nyakati  bora  kabisa  za  maisha  yao na utoto  wao," alisema.

"hawana  fedha, hawana  nyumba, samani  ama  hata  nguo kuondoka  navyo  kwasababu  ya mashambulizi  haya  ya  mabomu."

Kama  sehemu  ya  makubaliano na  kundi  la  Faylaq al-Rahman na  Urusi, wakaazi walipewa fursa  ya kubakia  mjini  Zamalka na  Arbin  wakati  eneo  hilo  likiangukia  katika udhibiti  wa  serikali.

lakini Abbas  alisema  hatabakia.

Syrien Krieg - Ostghuta bei Damaskus | Evakuierung aus Douma, Ostghuta
Raia kutoka Ghouta mashariki tayari wakiwa katika mabasi kupelekwa katika eneo linaloshikiliwa na waasi la IdlibPicha: Reuters/B. Khabieh

"Niliamua  kuondoka  Ghouta  kwasababu nawezaje  kuishi  pamoja  na  mtu ambaye  aliuwa familia  yangu, watoto watu, marafiki  zangu?  Na  mtu aliyeniharibu, maisha yangu, na hatima yangu?"

Tangu  kuanza mashambulizi Februari 18, raia  zaidi  ya  1,600  wameuwawa na  maelfu zaidi  wamejeruhiwa, kwa  mujibu  wa  shirika  linaloangalia  haki  za  binadamu  nchini  Syria.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Zainab Aziz