Wakongo kuhamishwa kuruhusu uchimbaji wa madini ya dhahabu | Masuala ya Jamii | DW | 23.07.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Wakongo kuhamishwa kuruhusu uchimbaji wa madini ya dhahabu

Haijabainika wazi ni kiasi gani cha fedha kitakacholipwa Wakongo hao kama fidia wakati watakapohamishwa kutoka maeneo yao

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila

Watu 15 elfu watahamishwa makwao ili kurahisisha uchimbaji wa madini ya dhahabu na kampuni ya Uingereza na Afrika ya Kusini ya ANGLOGOLD kwenye vijiji kadhaa vya vimbo la Orientale, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kampuni hiyo imeahidi kuwajengea makaazi mapya na kuunda ajira. Mradi huo umezusha tofauti kubwa baina ya serikali na mashirika ya kiraia ya jimbo hilo ambayo yamehisi kwamba hatua ya kuhamishwa kwa raia bila hiari yao inakiuka haki za binadamu, huku wanaharakati wa kimazingira wakionyesha pia wasiwasi wao kuhusu hatua hiyo ya serikali na kampuni ya Anglogold. Taarifa kamili na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo

Mwandishi:Saleh Mwanamilongo

Mhariri:Josephat Charo

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

 • Tarehe 23.07.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OTQx
 • Tarehe 23.07.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OTQx
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com