1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi wa kisomali wapata mjumbe maalumu

Josephat Charo Nyiro3 Oktoba 2016

Umoja wa Mataifa umemteua balozi wa zamani wa Kenya nchini Somalia, Mohamed Abdi Affey, kuwa mjumbe mpya maalumu kwa wakimbizi wa kisomali.

https://p.dw.com/p/2Qpva

Uamuzi huo unafuatia madai ya shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International kwamba Kenya inawalazimisha wakimbizi wa kisomali kurejea kwao katika jitihada za kuifunga kambi kubwa kabisa ya wakimbizi duniani ya Dadaab. Kenya inasema Wasomali wanarejea nchini kwao kwa hiari.  Katika Kinagaubaga, Naibu Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Josephat Charo, amezungumza na Mkurugenzi wa Shirika la wakimbizi la Danish Refugee Council, tawi la Kenya.