1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakili: Bobby Wine yuko katika hali mbaya

Lilian Mtono
17 Agosti 2018

Mbunge wa jimbo la Kyadondo (Chadondo) Mashariki nchini Uganda, Robert Kyagulani Ssentamu, maarufu Bobby Wine yuko kizuizini kwenye gereza la kijeshi nchini humo akituhumiwa kwa makosa matatu ya umiliki wa silaha kinyume cha sheria,

https://p.dw.com/p/33Iop

Lakini pia ushiriki wake kwenye machafuko katika eneo la Arua, yaliyochangia kushambuliwa kwa msafara wa magari ya rais Yoweri Museveni. Bobby Wyne alifikishwa katika mahakama ya kijeshi hapo jana, huku akisaidiwa na wanajeshi kwa kuwa alikuwa na hali mbaya ya kiafya kiasi ya kushindwa kutembea wala kuzungumza, kutokana na kipigo. Kuhusu hali yake na hatua zinazichukuliwa, Lilian Mtono amezungumza na wakili wake ambaye pia ni mbunge wa manispaa ya Bujiri, Asumani Basalirwa, na kwanza anazungumzia makosa yanayomkabili.