Wakenya washinda shindano la Mashujaa wa Mtaani | Matukio ya Afrika | DW | 15.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Wakenya washinda shindano la Mashujaa wa Mtaani

Washindi wa shindano la wanahabari la "Local Heroes Journalism Competition", lililodhaminiwa na Deutsche welle ikishirikiana na Shirika la habari la Standard Group wametunukiwa tuzo mjini Nairobi.

Joe Munene

Joe Munene Mkurugenzi wa matangazo wa shirika la vyombo vya habari la Standard mjini Nairobi.

Washindi hao wametunukiwa tuzo zao mjini Nairobi kwenye hafla iliyohudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Deutsche Peter Limbourg Welle ambaye yuko kwenye ziara ya Afrika kuitangaza idhaa mpya ya kimataifa ya televisheni ya DW News.

Jonathan Masongo mwanafunzi wa Mawasiliano na utangazaji katika chuo Kikuu cha Egerton huko Nakuru Kenya ndiye mshindi mkuu wa shindano hilo la Local Heroes Journalism Competition…

Kweye tuzo hiyo Jonathan atapata fursa ya kufanya kazi katika studio za Deutsche welle nchini Ujerumani kwa muda wa wiki mbili.

Kwa ujumla kumekuwa na washindi tisa wakiwemo washindi wa pili na tatu katika viwango vitatu vya Video, Sauti na Picha.

Carolyne Chepkoech Bii ameshinda tuzo ya ripoti bora zaidi ya redio…….

Akizungumza wakati wa hafla hilo, Mkurugenzi mkuu wa Deutsche Welle Peter Limbourg amesema, “Jioni ya leo nimefurahi kuona wanahabari chipukizi wenye vipaji na kazi nzuri walizotayarisha. Nadhani tunapasa kuendelea na mpango huu sijui hadi lini na mara ngapi na tufanye nchi zipi lakini wazo hili la kuangazia mashujaa mashinani katika anga ya kimataifa kupitia wanahabari naona ni wazo zuri.

Shindano hili limefanyika punde tu baada ya Deutche Welle kuanzisha Channel Mpya ya matangazo ya Televisheni kwa lugha ya Kiingereza hasa kwa Bara la Afrika.

“Ni hatua muhimu kwa Deutsche Welle kushughulikia maslahi ya watazamaji Barani Afrika kwa ubora zaidi kuliko tulivyokuwa tukifanya zamani. Ni mpango mzima wa kubadili mkakati ambapo Deutsche welle tungependa kuwapa watu wa bara la Afrika habari zinazowahusu kupitia chanel hii mpya ya Kiingereza”.

Shindano hilo limeendeshwa kwa ushirikiano na Shirika la Habari la Standard Group kupitia Redio Maisha.

“Ushirikiano wetu na DW hadi wakati huu umeendeshwa na kituo chetu cha Redio Maisha. Kituo ambacho tunakienzi kutokana na matokeo na thamani tunayowapa Wakenya” , Joe Munene Mkurugenzi wa Matangazo katika Shirika la Standard Group amesema katika ghafla hiyo.

Mnamo tarehe 22 mwezi Juni mwaka huu Deutsche Welle ilizindua kituo kipya cha matangazo ya Televisheni ya saa 24 ambacho kinapeperusha matangazo yake kwa lugha ya kiingereza kote duniani.

Mwandishi: Alfred Kiti / DW corespondent (Nairobi)

Mhariri: Josephat Charo