1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakalimani watatu wa kiafghani wameachiwa huru na wataliban hii leo

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxe

Kaboul:

Wataliban wanasema wamewaachia huru wakalimani watatu wa kiafghan waliotekwa nyara tangu mwezi uliopita pamoja na watumishi wawili wa kifaransa wa shirika la misaada ya kiutu Terre d’Enfance.Msemaji wa wataliban amesema mahabusi hao watatu wamekabidhiwa wazee wa kikabila katika mkoa wa kusini magharibi wa Nimroz.Wafanyakazi wawili wa shirika la Ufaransa la Terre d’Enfance wameshaachiwa huru.Wataliban waliitaka Ufaransa iwarejeshe nyumbani wanajeshi wake kutoka Afghanistan.