1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajerumani washangazwa na Mexico

Saumu Mwasimba
17 Juni 2018

Vijana wa Joachim Löw watolewa kamasi na Mexico kwa kupigwa bao 1-0 katika mchezo wao wa kwanza katika kundi F.Ni mechi iliyokuwa na msisimko mkubwa katika kipindi cha pili

https://p.dw.com/p/2zk13
Fußball WM 2018 Gruppe F Deutschland - Mexiko
Picha: Reuters/A. Schmidt

Wajerumani wametolewa kamasi katika mchezo wao wa kwanza kabisa katika kundi F dhidi ya  Mexico. Ujerumani imetandikwa bao 1-0 na Mexico katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo kunako dakika ya 34. Nderemo na shangwe zilitawala katika mechi hiyo ya kusisimua iliyoishia kwa wachezaji wawili wa timu ya Ujerumani kupigwa kadi za njano. Hirving Lazano ndiye aliyepiga mwakaju uliowachanganya wajerumani walioshindwa kurudi kwenye ramani ya mchezo katika kipindi cha mwanzo.

Fußball WM 2018 Gruppe F Deutschland - Mexiko
Picha: Reuters/M. Shemetov

Mexico wamewahi kuishinda Ujerumani mara moja katika mechi 11. Walishinda 2-0 katika mechi ya kirafiki mwaka 1985, lakini kocha wa Mexico Juan Carlos Osorio anaamini wachezaji wake wanapaswa kupuuza rekodi mbaya ya timu yake dhidi ya mabingwa wa dunia mara nne.

Goli la nahodha wa timu ya Serbia Aleksandar Kolarov katika dakika ya 59, limeipatia ushindi timu hiyo wa bao 1-0 dhidi ya Costa Rica kwenye mechi ya kwanza ya kundi E, mchana wa leo.

Costa Rica iliyofikia robo fainali ya michuano hiyo mwaka 2014, ilijitahidi kusawazisha goli lakini ilikosa nafasi nyingi za wazi. Mabingwa mara tano wa dunia Brazil inakwaana na Uswisi katika mechi nyingine ya kundi E baadae hii leo.