Wajerumani-Wamerakani wafikia milioni 50 | Masuala ya Jamii | DW | 02.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Wajerumani-Wamerakani wafikia milioni 50

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha nchini Marekani kuna raia wenye asili ya Ujerumani takribani milioni 50, na kufanya idadi yake kuwa kubwa kuliko kundi lingine lolote.

Hii inaitwa habari "mahususi kwa wakati muhimu", inaelezwa hivyo kwa kuwa katika kipindi hiki nchini Marekani, kuna marufuka kadhaa, kuna kutenguliwa taratibu fulani na hasa baada ya kuanza kwa utawala mpya wa Rais Danald Trump. Kuna masuala ya kuwapiga marufuku wasafiri na wahamiaji kutoka nchi saba za Kiislamu na la kusitisha progamu za upokezi wakimbizi. Na kwa maneno ya kihistoria ni kwamba idadi kubwa ya Wamarekani ni wahamiaji. Mfano halisi ni kuwa wenye asili ya Ujerumani, ndio yenye kufanya kundi kubwa kabisa la raia wa Marekani. Sensa ya wakazi ya mwisho kufanyika nchini humo inaonesha karibu watu milioni 50 nchini humo wana asili ya Ujerumani. Rekodi hiyo inaonesha nyongeza ya watu milioni sita zaidi ya ile ya kabla ya hapo. Pamoja na kulowea katika taifa hilo Wajerumani-Wamarekani wanaendeleza kuhifadhi historia yao. Mbali ya Wajerumani kufanya idadi ya raia milioni 50,wenye asili ya Irish milioni 35,Wamexico miloni 31 na wenye asili ya Uingereza milioni 27. Kwa ujumla kuna zaidi ya Wamerakani karibu milioni 320. Lakini kwa upande wa Wajaerumani-Wamarekani asilimia kumi miongoni mwao wanazungumza au kukielewa Kijerumani, wakiwemo watu maarufu kama Sandra Bullok, Henry Kissinger au Leonardo DiCaprio na ndugu wa karibu wa rais Donald Trump. Kwa jumla wote wa wenye uwezo huo wanakadiriwa kufikia milioni tano. Jamii hiyo ya watu inalengwa na vyombo madhubuti vya kama magazeti 100 na majarida mengine, kiasi kingine cha radio 100 na televisheni 20. Lakini ni muhimu ulimwengu ukajua kuwa Marekani ina gazeti kongwe kabisa la kila juma la Kijerumani "New Yorker Staats-Zeitung" lilianza kuchapishwa 1834.

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Saumu Mwasimba

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com