Waislamu watakiwa kulaani kundi la Dola la Kiislamu | Magazetini | DW | 07.10.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Waislamu watakiwa kulaani kundi la Dola la Kiislamu

Waislamu nchini Ujerumani wanavyochukua hatua dhidi ya wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu , mjadala juu ya kulijenga upya jeshi la Ujerumani, na mkutano wa maaskofu wa kanisa Katoliki.

Veranstaltung Unter dem Motto: Muslime stehen auf gegen Hass und Unrecht

Waislamu nchini Ujerumani

Gazeti la Mittelbayerische Zeitung likiandika kuhusu jamii ya Waislamu nchini Ujerumani. Gazeti linaandika.

"Wiki chache zilizopita Waislamu walionesha mshikamano wao na Wapalestina pale Israel ilipokuwa ikilishambulia eneo la Gaza kwa mashambulizi ya jeshi la ardhini na angani. Mhariri anauliza kwanini wakati huu ambapo kuna mauaji ya kinyama mbele ya kamera na kitisho cha mauaji ya halaiki kinachofanywa na kundi la IS linalotumia dini hiyo kwa manufaa yao na kufanya ugaidi hakuna hatua zinazochukuliwa? Ndio sababu tunasema , Waislamu , inachukiza mhariri anaandika.

Uislamu kama dini nyingine ni muongozo wa maisha ya kuishi pamoja, kwa ajili ya maisha bora. Kama ilivyo kwa chuki dhidi ya Wayahudi , pia chuki dhidi ya Uislamu ni tatizo kubwa kwa jamii. Iwapo Uislamu ni sehemu ya Ujerumani , unaweza pia kuwa suluhisho na ni lazima kuchukua hatua."

Nalo gazeti la Freie Presse likizungumzia kuhusu mada hiyo limeandika:

"Ugaidi unaofanywa kwa jila la Allah unavutia tu jamii masikini na kupoteza maisha ya hapa duniani , na kutokana na imani hii potofu kilitekelezwa kitendo cha ugaidi Septemba 2001. Katika dunia hii inayotegemea masuala ya kiuchumi, ambapo vijana wanaweza kuvutika kwa haraka ,inaonekana kuwa rahisi kuwashawishi na kwamba kujiunga na vita kunaleta manufaa. Hii haina tofauti na washika bendera ya kundi la Dola la Kiislamu kama ilivyo kwa wanazi mamboleo."

Bundesverteidigungsministerin Ursula von der Leyen 2014

Waziri wa ulinzi Ursula von der Leyen

Kuhusu mradi wa kujenga upya jeshi imara la Ujerumani , mhariri wa gazeti la Nürnberger Nachrichten anaandika.

"Itakuwa shauku kubwa kuona waziri Ursula von der Leyen kutoka chama cha CDU kwa ushauri wa wataalamu anatakavyoanza maelezo yake. Baadhi ya sentensi zitasikika kama vile mapigo ya fimbo katika masikio. Utaratibu wa kushughulikia mradi wa ujenzi mpya wa jeshi la Ujerumani utahitaji utamaduni wa uongozi, ambamo kutakuwa na uwazi na uadilifu. Hii ina maana , hali hiyo hadi sasa haipo."

Gazeti la General - Anzeiger la mjini Bonn , kuhusu mada hiyo limeandika.

"Jeshi la Ujerumani linalazimika haraka kufanyia kazi masuala fulani kwa wakati mmoja na sio moja baada ya jingine. Jeshi linapaswa kila siku kuonesha uwezo wa kufanyakazi, hatimaye linapaswa kuacha malalamiko na mivutano kuhusu gharama za kulipatia silaha mpya , na pia pande zote zinapaswa kuacha kutoa visingizio vya kulitoa jeshi hilo katika majukumu ya kimataifa."

Mhariri wa gazeti la Saabrücker Zeitung anazungumzia kuhusu mkutano wa maaskofu wa kanisa Katoliki mjini Vatican. Mhariri anaandika:

Vatikan Auftakt Bischofssynode 05.10.2014 Papst Franziskus

Papa Francis wa kanisa Katoliki

"Kiongozi wa kanisa Katoliki , Papa Francis ameleta hali mpya katika kanisa hilo. Lakini ni kwanini ameonesha tu hadi sasa hali ya matarajio ya kukisia tu kuhusiana na masuala mazito yenye mivutano katika kanisa kama ndoa na maisha ya ngono? Lengo la kuanzisha mjadala papa Francis amekwisha lifikia.

Katika miaka ya nyuma ni mara chache kumekuwa na majadiliano ya wazi na magumu kuhusu mwelekeo wa kanisa . Hatua iliyofikiwa sasa ni mafanikio kwa papa Francis. Hata hivyo anaingia katika hatua yenye shaka kubwa. Iwapo wengi wa maaskofu wataamua kutolifungua kanisa hilo, wengi wa waumini watavunjika moyo."

Mwandishi : Sekione Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman