Wahindu washambuliana na Wakristo India | Habari za Ulimwengu | DW | 28.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Wahindu washambuliana na Wakristo India

NEW DELHI

Huko mashariki mwa India kumekuwepo na repoti ya kuzuka kwa ghasia kati ya wafuasi wa Kihindu na Wakristo.

Makanisa 11 yameunguzwa moto wafuasi wa sera kali za mrengo wa kulia wa Kihindu au Mabaniyani katika wilaya ya Khandamal kwenye jimbo la Orissa.Wanamgambo wa Kikristo baadae walifanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya nyumba za Wahindu.

Mvutano huo wa karibuni umepamba moto baada ya kundi la Wakristo kudaiwa kumshambulia kiongozi wa kundi la mrengo wa kulia Vishwa Hindu Parishad VHP ambaye analiongoza kundi hilo kupinga kubadilishwa watu dini kuwa Wakristo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com