1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji elfu 12 waingia Slovenia

Admin.WagnerD22 Oktoba 2015

Zaidi ya wahamiaji 12, 600 wamewasili nchini Slovenia katika kipindi cha masaa 24. Idadi hiyo inapindukia ile ya walioingia Hungary katika wakati wa kilele cha mgogoro wa wimbi wahamiaji mwezi cha Septemba.

https://p.dw.com/p/1GsWa
Slowenien Flüchtlinge bei Rigonce
Idadi kubwa wakimbizi wakiwa wanasubiri hatma yao nchini SloveniaPicha: Reuters/S. Zivulovic

Kwa mujibu wa jeshi la polisi mpaka wakati huu zaidi ya wahamiaji 34,131 wameingia Slovenia tangu Jumamosi iliyopita, wakati ambapo wimbi hilo la wakimbizi lilipoanza. Siku zilizopita waliingia jumla ya wahamiaji 21,455 na sasa kumekuwa na ongezeko hilo la watu 12,676.

Mwezi uliopita, Septemba 23, Hungary,ambayo tangu wakati huo ilifunga mipaka yake iliweka rekodi ya kuwapokea wakimbizi 10,046 kwa siku moja. Hata hivyo hali bado tete kwa Slovenia, taifa lenye jumlam ya watu milioni mbili ambalo leo hii vilevile linatarajiwa kundi lingine la wahamiaji wapatao 10,000. Idadi hiyo ya wakimbizi ipo katika jitahada kubwa za harakati za kuingia eneo la kaskazini mwa Ulaya kabla ya msimu wa baridi.

Wahamiaji kuingia zaidi Slovenia

Jeshi la polisi limesema asubuhi ya leo, kwa sekta mojaa pekee kati ya wahamiaji 2,000 na 3,000 walitarajiwa kuingia Slovenia, kutoka Croatia. Katika kukabiliana na hali hiyo mapema jana Bunge la Slovenia limelipa nguvu zaidi jeshi kwa askari wake kujiunga na polisi wa katika maeneo ya mpaka wake na Croatia kupiga doria katika eneo la umbali wa kilometa 670.

Slowenien Flüchtlinge bei Dobova
Wakimbizi wakiwa wamezuiwa mjini DebovaPicha: picture-alliance/AP Photo/D. Bandic

Serikali ya Slovenia vilevile imetoa ukosoaji mkali kwa Croatia, kutokana na uamuzi wake wa kufungua mpaka wake Jumatatu usiku na kuruhusu idadi kubwa ya wahamiaji hao kuingia nchini mwake.

Hungary yatoa tamko

Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban amewataka viongozi wa Umoja wa Ulaya kuzifanyia marekebisho sera zake kuihusu uhamiaji na kuwahusisha wapiga kura kujadili kuhusu hatma ya baadae ya ya bara lao, kwa kusema kinyume chake wataweza kukabiliana na mgogoro wa kisiasa na kusababisha kitisha cha matakwa ya demokrasia.

Hungary imeshughulikia wimbi la wahamiaji barani Ulaya kwa kujingea uzio wa chuma katika mpaka wake na mataifa ya Serbia na Croatia, hatua ambayo imepokelewa kwa namna tofauti na viongozi wa mataifa ya Ulaya, wapo waliopokea vyema na wapo walioikosoa vikali.

Umoja wa Ulaya umeitisha jumapili ijayo mkutano mdogo wa kilele na mataifa ya Balkan mjini Brussels kuhusu mgogoro wa uhamiaji. Bara la Ulaya kwa wakati huu lipo katika jitahada za kutafuta suluhu ya pamoja katika kukabiliana na janga hilo lubwa kabisa kuhiwahi kutokea tangu 1945.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa zaidi ya wahamiaji na wakimbizi 600,000 , wengi wao wakitokea maeneo yenye machafuko huko Syria, Iraq, na Afghanistan wamekuwa wakifanya safari zenye kuhatarshia maisha yao za kuingia ulaya kwa mwaka huu pekee.

Mwandishi: Sudi Mnette/RTR/AFPE
Mhariri:Hamidou Oummilkheir