1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahafidhina waongoza katika uchaguzi wa bunge Iran

15 Machi 2008

-

https://p.dw.com/p/DOl2

TEHRAN

Matokeo ya mwanzo katika uchaguzi wa bunge nchini Iran yaliyotangazwa na vyombo vya habari nchini humo yanaonyesha wahafidhina wanaongoza ingawa wanaopendelea mageuzi pia wamepata viti kadhaa katika maeneo bunge mbali mbali ya nchi.

Kuna viti 290 vya bunge vinavyogombewa,ambapo viti 260 vinagombewa katika miji ya mikoani na vingine 30 vinagombea kwenye mji mkuu Tehran.Kwa mujibu wa ripoti zilitolewa na shirika la habari la Fars ambalo linahusishwa na serikali,wenye msimamo mkali wamejinyakulia viti katika miji ya Bam kusini mashariki mwa mkoa wa Kerman,Nain kwenye mkoa wa Isfahan pamoja na Boroujen na Farsan.Katika uchaguzi huu wa bunge wapinzani wengi wa rais Mahmoud Ahmedinejad walizuiwa kugombea.Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imepinga uchaguzi huo ikisema matokeo hayatakuwa ya haki kutokana na wapiga kura kunyimwa uhuru kamili wa kujichagulia wanaowataka.Serikali ya Iran iliwatolea mwito wapiga kura kujitokeza kwa wingi ili kuzithibitishia nchi za magharibi kwamba mfumo wake wa Uchaguzi unakubalika na wananchi,aidha muda wa kupiga kura uliongezwa kwa saa mbili.