1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa wa Kipalestina waongeza madai

14 Mei 2012

Wafungwa wa Kipalestina walio katika mgomo wa kutokula wameongeza masharti zaidi ili kusitisha mgomo wao unaowahusisha wafungwa 1,550 na mahabusi wawili unaoendelea kwa siku ya 76 sasa. .

https://p.dw.com/p/14vN3
Waandamanaji wa Kipalestina wakiwa na mabango
Waandamanaji wa Kipalestina wakiwa na mabangoPicha: picture alliance / landov

Wafungwa na mahabusu hao wameutaka utawala wa Israel uregeze masharti kwa kuruhusu ndugu zao wawatembelee gerezani, ruhusa ya kupata elimu, kuondolewa kwa utaribu wa kumuweka mtu kizuizini bila ya kufunguliwa mashitaka.

Kukiwa na makubaliano ya Cairo juu mgomo huo baina ya Israel, mawakili wa wafungwa na Misri, hali bado tete, huku wafungwa wakiwa katika mgomo. Mara baada ya makubalinao ya Cairo kufikiwa, wafungwa wenyewe ndiyo wenye mamlaka ya kukubali makubalinao au la.

Hiane Tasmini, ambaye ni mwanasheria kutoka Taasis moja huko Gaza anasema

"Mgomo wa kula ni matokeo ya mwisho ya kujikomboa, ni kujiumiza sana kunaweza kusababisha kifo, kwa sasa ndiyo njia ya kujikomboa kwa wafungwa hao wa Kipalestina."

Inataraijiwa viongozi wa Magereza watakutana na wafungwa hao kuwaeleza makubalino na wao kutoa msimamo wao baada ya maelewano ya pande zote mbili. Kukiwa na mahabusu wengi waliwekwa rumande bila ya kufunguliwa mashitaka kuanzia miezi sita na wengine miaka kadhaa kwa amri hiyo ya kuwekwa kizuizini.

Baadhi ya wanachama wa chama kimoja cha siasa cha Palestina
Baadhi ya wanachama wa chama kimoja cha siasa cha PalestinaPicha: AP

Mahabusu Diab na Halahla

Bilal Diab na Thael Halahla ambao nao ni miongoni mwa waliomo katika mgomo huo wakipinga kuwekwa kwao kizuizini bila ya mashitaka. Jamil Khatib, ambaye ni wakili wa mahabusu hao, ameliambia Shirika la habari la Ufaransa, AFP, kuwa Israel imekubali hitaji la mahabusu na wafungwa hao, lakini kikubwa ni maamuzi ya kila mmoja na shauri la kuendelea na mgomo au kuacha mgomo limo kwao.

Wakili huyo anasema bayana kuwa utawala wa Israel unaweza kuwachezea shere kwa kuwaandikia vibali vipya vya kuwaweka kizuizini tu, hakuna litakalofanyika zaidi.

Waziri wa Palestina asema masharti yote yamekubaliwa

Kwa upande wake, waziri wa Magereza wa Palestina, Issa Qaraqaa ana imani na makubalinao hayo kwani ameimbia Redio ya Palestina kuwa maombi muhimu karibu yote yameafikiwa na Israel.

Mapema waziri mkuu wa Palestina, Mahmud Abbas, ameionya Israel kama mfungwa mmoja akifariki tu kwa mgomo huo ameapa kuwa janga la kitaifa, akisema wazi kuwa wafungwa na mahabusu wanayo haki ya kudai haki zao.

Israel itatoa taarifa

Kwa upande wake, msemaji wa magereza wa Israel hakuweka bayana juu ya kilichoafikiwa katika makubaliano hayo, Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamini Netanyau, ikisema kuwa punde italitolea maelezo suala hili.

Picha ya Ahmed Saadat mjini Ramallah katika maandamano
Picha ya Ahmed Saadat mjini Ramallah katika maandamanoPicha: AP

Mwezi mmoja uliopita Serikali ya Israel ilimwacha huru kiongozi wa Kikundi cha Kiislamu cha Jihad, Khader Adnan, ambaye alikubali kuacha mgomo huo katika siku ya 66, huku kukiwa na maandamano makubwa Gaza ya kuwaunga mkono wafungwa katika mgomo huo.

Mwandishi:Adeladius Makwega/RTRE&AFPE.

Mhariri: Miraji Othman