1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafauasi wa Sadr wapiga kura ya maoni

2 Aprili 2010

<p>Nchini Iraq, wafuasi wa kiongozi wa dini wa madhehebu ya Kishia, Muqtada al-Sadr, leo wamejitokeza kupiga kura ya maoni katika zoezi la siku mbili la kumchagua waziri mkuu mpya wa nchi hiyo.</p>

https://p.dw.com/p/MmIa
Former Iraqi Prime Minister Ayad Allawi speaks to his supporters after the full election results released Friday for Iraq's 325-seat parliament show Allawi winning 91 seats, edging out Prime Minister Nouri al-Maliki's 89 seats in Baghdad, Iraq, Friday, March 26, 2010. (AP Photo/ Khalid Mohammed)
Waziri Mkuu wa zamani wa Iraq, Ayad Allawi akizungumza na wafuasi wake baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa bunge.Picha: AP

Wafuasi wa muungano wa vyama vya kidini vya Kishia "Iraqi National Alliance" kwa maelfu, wameanza kupiga kura ya maoni kuamua nani atakaeiongoza Iraq. Uchaguzi wa bunge uliofanywa Machi 7 haukupata mshindi wa moja kwa moja. Kura ya maoni inayopigwa leo na kesho Jumamosi haina nguvu ya  kisheria. Lakini kwa wengi, hiyo ni njia inayotumiwa na  Muqtada Sadr kumuunga mkono ye yote mwingine isipokuwa adui wake mkubwa, Waziri Mkuu wa hivi sasa, Nuri al-Maliki. Ili kuweza kubakia madarakani, al Maliki asiependwa na wafuasi wa Sadr, anahitaji kuungwa mkono na Washia wengi.

Chama cha Iraqiya cha Ayad Allawi kinachotenganisha dini na siasa, kimeshinda viti 91. Chama cha State of Law Alliance kinachounganisha  makundi ya Kishia na kuongozwa na al-Maliki kimepata viti 89.  Nafasi ya tatu imechukuliwa na Iraqi National Alliance baada ya kushinda viti 70. Hakuna aliepata wingi wa kuweza kuunda serikali peke yake. Lakini Allawi na al-Maliki wanadai kuwa na haki ya kuunda serikali mpya na hivi sasa wanajadiliana na vyama vingine. Kila mmoja wao anahangaika kuwa wa kwanza kufanikiwa kuunda serikali mpya.

Sasa, wagombea wakuu wawili, Allawi na al-Maliki, ndio wanapigania kupata kura za wafuasi wa Muqtada al Sadr katika kura ya maoni isiyo rasmi. Hata Ibrahim al-Jaafari aliekuwa waziri mkuu kabla ya al-Maliki, yupo katika orodha ya wagombea wadhifa huo. Makamu wa Rais Adel Abdel Mahdi na Jaafar al-Sadr mtoto wa mwaasisi wa chama cha al-Maliki cha "Islamic Dawa Party" vile vile ni miongoni mwa wagombea hao.

Uhasimu wa wagombea hao umevuka misingi yao ya kidini, hasa kwa sababu ya operesheni ya kijeshi ya mwaka 2008 iliyoamriwa na al-Maliki dhidi ya Jeshi la Mahdi ambalo ni tawi la kijeshi la chama cha Sadr. Matokeo ya kura ya maoni inayopigwa leo na kesho, yanatazamiwa kutangazwa siku ya Jumatatu.

Mwandishi:Martin,Prema/DPAE/AFPE

Mhariri: Othman,Miraji