1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafauasi 7 wa Muslim Brotherhood wakamatwa Misri

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CRtE

Polisi nchini Misri,imewakamata wanachama 7 wa upinzani wa Muslim Brotherhood.Hiyo ni sehemu ya wimbi la kuwakamata wanachama wa Muslim Brotherhood hasa katika Bonde la Mto Nile.Mwezi huu peke yake zaidi ya wanachama 50 wa kundi hilo la itikadi kali za kiislamu,wamekamatwa katika eneo hilo ambako kundi hilo linaungwa mkono na wengi.

Chama cha Muslim Brotherhood kisichotumia nguvu,ni kundi kuu la upinzani nchini Misri na linagombea kuwa na taifa la Kiislamu kwa njia ya kidemokrasia. Chama hicho kinaendelea na shughuli zake wazi wazi,licha ya kupigwa marufuku tangu mwongo mmoja uliopita.Hivi sasa,zaidi ya wanachama 200 wa kundi hilo wapo kizuizini.