Wafanyakazi wa shirika la kujitolea waliohukumiwa kwa kuwateka nyara watoto watarejeshwa Ufaransa | Habari za Ulimwengu | DW | 28.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Wafanyakazi wa shirika la kujitolea waliohukumiwa kwa kuwateka nyara watoto watarejeshwa Ufaransa

NDJAMENA:

Wafanya kazi za misaada sita ambao walihukumiwa miaka minane kila mmoja nchini chad, kwa kuwateka nyara watoto 103 watarudishwa nyumbani kwao Ufaransa kutumikia kifungo chao huko.

Serikali ya Ufaransa imeiomba Chad kuwarejesha nyumbani wanaume wanne na wanawake wawili.

Walikuwa wanatumikia shirika lisilolaserikali la Zoe’s Ark.Watu hao watarejeshwa Ufaransa kulingana na mkataba wa kisheria wa nchi hizo mbili wa mwaka 1976.

Wafanya kazi hao walidai kuwa walikuwa wanasaidia kuwaokoa watoto hao mayatima,hata hivyo watoto karibu wote walikuwa wametoka katika familia ambazo baado ni hai na kuwa walishawishiwa kutoa watoto hao kwa ajili ya kupelekwa Ufaransa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com