1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waendesha mashtaka wataka vifungo dhidi ya rais wa Barcelona

23 Machi 2015

Waendesha mashtaka wa Uhispania wanaomba vifungo vya miaka miwili na miezi mitatu jela dhidi ya rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu na miaka saba dhidi ya Sandro Rosell, kuhusiana na sakata la Neymar

https://p.dw.com/p/1Evfb
FC Barcelona Rücktritt Präsident Sandro Rosell
Picha: Reuters

Mahakama ya Madrid pia inata klabu hiyo itozwe faini ya euro milioni 22.2. kuhusiana na uhamisho wa Neymar ambayo umekuwa ukifanyiwa uchunguzi wa ufisadi.

Watu hao wawili pamoja na klabu walishtakiwa kwa kukwepa kulipa kodi na Rosell pia anatuhumiwa kwa dosari za matumizi ya fedha wakati akiwa uongozini.

Baada ya miezi kadhaa ya upelelezi, jaji wa mahakama ya Uhispania sasa lazima afanye uamuzi kama mashtaka yataanza rasmi.

Barcelona ilisema ililipa jumla ya euro milioni 57 ili kuipata sahihi ya Neymar kutoka klabu ya Santos nchini Brazil, lakini jaji anashuku kuwa kiasi kamili cha fedha kilikuwa zaidi ya euro milioni 83.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Abdulrahman