1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachezaji wawili wa Hoffenheim wameambukizwa Corona

16 Oktoba 2020

Siku ya ijumaa Hoffenheim imetoa taarifa, wachezaji wawili wameambukizwa Covid-19 na mwengine mmoja yupo karantini. Haya yamejiri mara tu baada ya kutoka kwa mechi za Kitaifa.

https://p.dw.com/p/3k25F
Deutschland Sinsheim | Bundesliga | Tor für TSG 1899 Hoffenheim
Wachezaji wa Hoffenheim wakishangilia baada ya kufunga bao.Picha: Wolfgang Rattay/Reuters

Hoffenheim siku ya jumamosi itashuka dimbani kuchuana na Borrusia Dortmund. Wachezaji hao wawili hawakutajwa majina yao, wamerudi kutoka katika nchi zao kushiriki katika michuano ya mataiafa, hata hivyo wawili hao hawakutangamana na wachezaji wengine wala wafanyakazi. 

Aidha klubu ya Hoffenheim katika taarifa yake  imesema mchezaji aliye karantini ni kutokana na mmoja wa familia yake kupatika na Covid-19.

Wachezaji kadhaa wa Hoffenheim walisafiri kwa mechi za kimataifa pamoja huku Andrej Kramaric anayeichezea Croatia akiwa mfungaji bora wa ligi hiyo akiwa na mabao sita.

FIFA Fußball-WM 2018 in Russland | Andrej Kramaric, Kroatien
Picha: Reuters/M. Shemetov

Kutokana na ongezeko la viwango vya maambukizo ya covid-19  Ujerumani,mechi kati ya Augsburg v RB Leipzig Jumamosi itachezwa bila mashabiki uwanjani. Arminia Bielefeld nao watawakaribisha mabingwa watetezi Bayern Munich mbele mashabiki wasiozidi 300.

Mechi ya Borussia Moenchengladbach dhidi ya Wolfsburg Jumamosi itakuwa pia itahudhuuriwa na mashabiki 300 pekee, Freiburg dhidi ya Werder Bremen haitokuwa na shabiki hata mmoja uwanjani.

Katika jedwali la Bundesliga Hoffeinheim ipo na alama 6 sawia na Dotmund baada ya kucheza mechi tatu.

RTRE/Dpa