1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachezaji wasiochanjwa kutolipwa mishahara

Sylvia Mwehozi
23 Novemba 2021

Klabu ya soka ya Hertha Berlin inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, imesema haitowalipa mishahara wachezaji ambao hawajachanjwa dhidi ya virusi vya corona kipindi wakiwa Karantini.

https://p.dw.com/p/43Mj0
Fußball Bundesliga Hertha BSC v Bayer 04 Leverkusen
Picha: ANNEGRET HILSE/REUTERS

Klabu ya soka ya Hertha Berlin inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, imesema haitowalipa mishahara wachezaji ambao hawajachanjwa dhidi ya virusi vya corona kipindi wakiwa Karantini.

Ripoti za vyombo vya habari zinasema pia klabu ya Byaern Munich imeanza utekelezaji wa sera kama hiyo katikati mwa mjadala mkubwa unaomhusu mchezaji Joshua Kimmich ambaye hajachanjwa.

Mkurugenzi wa Hertha Berlin Fredi Bobic amenukuliwa akisema kuwa "tayari tumeamua kwamba kuanzia Novemba 2, wachezaji wasiochanjwa hawatolipwa mishahara yao wakati watakapokuwa karantini".

Klabu ya Hertha imeathirika mara kadhaa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona lakini ripoti zinasema karibu wachezaji wote wamechanjwa. Mwanzoni mwa Oktoba, klabu hiyo ilisema wachezaji wasiochanjwa wangejilipia wenyewe vipimo vya corona.