Wachambuzi wauzungumzia mkutano wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika kuhusu DRC | Media Center | DW | 23.01.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Media Center

Wachambuzi wauzungumzia mkutano wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika kuhusu DRC

Sikiliza sauti 02:56

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inajiandaa kumuapisha rais wake mpya Felix Tshisekedi wiki hii baada ya kinyang'anyiro kikali cha uchaguzi ambao matokeo yake yalipingwa na mgombea aliyeshika nafasi ya pili, Martin Fayulu. Lakini hapo jana katika mkutano ulioandaliwa mjini Brussels, Ubelgiji, viongozi wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika waliashiria kuwa watafanya kazi na rais mteule licha ya kwamba hawakumpongeza moja kwa moja kwa ushindi wake. Je, ni kwa nini viongozi wa AU walikwenda Brussels kujadili matokeo ya uchaguzi wa Kongo na ilhali hawajahi kufanya hivyo katika chaguzi za mataifa mengine ya Afrika yaliyokumbwa na utata? Sikiliza mahojiano kati ya Bruce Amani na mchambuzi wa masuala ya siasa kutoka nchini Tanzania, Profesa Mwesiga Baregu.