1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa waidhinisha hati ya kudhibiti maambukizi

Sudi Mnette
26 Julai 2021

Wakati wabunge wa Ufaransa wakiridhia muswaada utakaowalizimisha wafanyakazi wa sekta ya afya kuchanja chanjo ya Covid-19, wabunge wa Ujerumani wapo katika mabishano makubwa juu ya chanjo hiyo iwe lazima kwa umma au la.

https://p.dw.com/p/3y2Wv
Eröffnung der Konferenz zur Zukunft Europas - Emmanuel Macron
Picha: ElyxandroCegarra/Panoramic/imago images

Bunge la Ufaransa leo hii limeridhia muswada ambao utafanya chanjo ya Covid-19 kuwa ya lazima kwa wafanyakazi katika sekta ya afya pamoja na takwa la kuizoingezea nguvu hati maalumu za kuingilia katika maeneo ya kijamii ya wazi.

Hatua hiyo inaridhiwa wakati Ufaransa ikikabiliana na wimbi la nne la maambukizi ya virusi vya corona. Tayari wanaohudhuria katika majumba ya makumbusho, sinema au mabwawa ya kuogelea wanazuiwa kuingia katika maeneo hayo kama hawataonesha vithibitisho vya kupata chanjo ya Covid-19 au kufanya vipimo vya karibuni kabisa dhidi ya virusi vya corona.

Huwezi kuingia katika maeneo ya wazi na ya kijamii.

Corona-Protest in Frankreich
Wapinga vizuizi vya Covid-19 UfaransaPicha: Florent Moreau/MAXPPP/dpa/picture alliance

Vithibitisho hivyo kwa kiwango kikubwa vinahitajika katika matamasha au katika vilabu vya starehe. Lakini kwa sasa kuanzia mwezi ujao wa Agosti, nyaraka hizo zitahitajika zaidi katika kuingia katika migahawa, baa, na pia kwa safari za muda mrefu za treni na ndege.

Kama ilivyo kwa mataifa mengine ya Ulaya, Ufaransa ipo katika makabliano na kizazi kingine cha virusi vya corona aina ya Delta ambacho kinaambukiza kwa kwa kasi. Kirusi hicho ambacho kimegudulika kwa mara ya kwanza nchini India, kinatishia kuongeza muda zaidi wa makabiliano ya janga la corona na kufifisha jitihada za mataifa katika kufufua uchumi.

Kumekuwa na mgawanyika mkali kwa wanasiasa nchini Ujerumani iliotokana na onyo la kiongozi wa wafanyikazi katika ofisi ya Kansela wa Ujerumani, ambae amenukuliwa akisema vizuizi kwa watu wasiochanja vinaweza kuwa muhimu kama viwango vya maambukizi ya virusi vya corona vitakuwa na ongezeko kubwa jipya katika miezi ijayo.

Wanasiasa wa Ujerumani wanabishana kuhusu ulazima wa chanjo kwa umma.

Mkuu huyo, Helge Braun aliliambia gazeti la kila Jumapili la hapa Ujerumani la Bild am Sonntag kwamba, hatarajii vizuizi vyoyote vipya vinavyohusisha na makabiliano dhidi ya ongezeko la maambukizi nchini Ujerumani. Lakini akaenda umbali wa kusema watu wasiochanja wanaweza kuzuiwa kuingia katika maeneo kama ya migahawa, kumbi za sinema na viwanja vya michezo kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa hatari za maambukizi.

Kauli yake hiyo imeibua mijadala mikali katika siasa za Ujerumani na hata ndani ya chama Kansela Merkel cha CDU. Mgombea wa chama hicho kwa nafasi ya ukansela ambae anatarajiwa kumrithi Merkel, Armin Laschet amesema anaipinga aina yoyote rasmi au isiyo rasmi ya kuwalazimisha watu kuchanja kwa wakati huu.

Zaidi ya asilimia 60 ya idadi jumla ya watu nchini Ujerumani imepata japo chanjo moja ya Covid-19 wakati asilimia nyingine 49 imekamilisha chanjo zote mbili.

Kwengineko barani Afrika, wakati Ghana inatarajiwa kupkea zaidi ya dozi milioni 18 za virusi vya corona kabla ya Oktoba, katika kipindi hiki ambacho taifa hilo linakabiliana na wimbi la wimbi la tatu la virusi vya corona, Afrika Kusini imeondoa marufuku ya kuuza kwa vileo katikati mwa juma na kuruhusu watu kusafiri kutoka jimbo moja kwenda lingine.

Vyanzo: AP/RTR/AFP