1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge Afrika Kusini wanataka ufugaji wa simba usitishwe

Sekione Kitojo
27 Novemba 2018

Wabunge nchini Afrika Kusini wanataka kusitisha ufugaji wa simba. Afrika Kusini ina zaidi ya simba 8,000 wanaofugwa kwa ajili ya kuwinda, biashara ya mifupa yao, utalii na kwa ajili ya shughuli za utafiti.

https://p.dw.com/p/38y6y
Indianapolis  Zoo - Löwin tötet Löwen in amerikanischem Zoo
Picha: picture-alliance/dpa/AP/Indianapolis Zoo

Wabunge nchini Afrika Kusini wanataka kusitisha ufugaji wa simba kwa ajili ya uwindaji pamoja na kufanya biashara  ya  mifupa  yao, na kuliweka bunge katika mvutano na wafanyabiashara wenye nguvu wa shughuli hiyo.

Afrika  Kusini  ina  zaidi  ya  simba  8,000  wanaofugwa ambao  wanazalishwa  kwa  ajili  ya  kuwinda, biashara  ya mifupa  yao, utalii  na  kwa  ajili  ya  shughuli  za  utafiti, kwa  mujibu  wa  makadirio  ya  makundi  ya  hifadhi  ya wanyama.

Kwa  ulinganisho  kuna  simba  3,000  wanaoishi  porini wanaoishi  katika  mbuga  za   taifa  ambako uwindaji umepigwa  marufuku.

Kamati  ya  wabunge  inayohusika  na  masuala  ya mazingira imependekeza  Novemba  12  kwamba  serikali ifikirie upya  kuhusu  sheria  zinazohusiana  na  uzalishaji wa  simba  wanaofugwa  kwa  ajili  ya  uwindaji na biashara  ya  mifupa  yao.