1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge 17 waponea kutimuliwa Tanzania

3 Julai 2018

Rais wa Tanzania John Magufuli amesema wabunge wa majimbo 17 ya Kusini mwa Tanzania kunakolimwa zao la korosho wangeweza kufukuzwa kazi kama wangepinga mapendekezo ya serikali na kukwamisha Sheria ya Bajeti 2018.

https://p.dw.com/p/30jW5
Rais wa Tanzania, John Magufuli
Picha: picture alliance/AA/M. Mukami

J03.07.2018Tanzania: Magufulis speech - MP3-Stereo

Nchini Tanzania mjadala mkubwa ni kile alichokizungumza rais wa taifa hilo John Pombe Magufuli jana kuhusu sakata la madai ya fedha za kilimo cha korosho bungeni kwenye hafla ya kuwaapisha mawaziri na manaibu katibu mkuu aliowateuwa juzi kufuatia kile kilichoitwa mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri. Kutoka mjini Mwanza, DW imezungumza na mchambuzi wa siasa za Tanzania, Marcell Hamduni, kwanza kutaka kujua nini tathimini yake kwa kauli ya rais wa Tanzania.