Waasi waunda chama kipya mashariki mwa Kongo | Matukio ya Afrika | DW | 08.05.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Waasi waunda chama kipya mashariki mwa Kongo

Wapiganaji wa zamani wa chama cha waasi, CNDP, waliojiondoa katika jeshi la DRC, wakati ambapo wanapambana na jeshi la nchi hiyo kwa zaidi ya wiki moja sasa, leo08.05.2012 wametangaza kuundwa kwa chama kipya cha waasi.

Waasi wa mashariki ya Kongo

Waasi wa mashariki ya Kongo

Chama hicho kimeundwa na viongozi wa ngazi ya juu wa zamani wa waasi wa Chama cha CNDP na kinaongozwa na Kanali Makenga Sultani, naibu kamanda wa zamani wa CNDP kabla ya wapiganaji wa chama hicho kujiunga na jeshi la DRC hapo Januari 2009. Kuundwa kwa chama hicho kunadhaniwa kuwa huenda kutasababisha vurugu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kuendelea.

John Kanyunyu, mwandishi wetu katika eneo hilo, ametutumia ripoti ifuatayo kutoka Goma

(Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: John Kanyunyu

Mhariri: Othman Miraji


Sauti na Vidio Kuhusu Mada