1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa zamani wa SPLM warejea serikalini

27 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CgtI

KHATOUM.Waasi wa zamani wa kusini mwa Sudan wamerejea katika serikali ya nchi hiyo miezi miwili baada ya kujitoa kutokana na kutoelewana katika utekelezaji wa mkataba wa amani uliyohitimisha miongo miwili ya vita.

Hatua hiyo ya kurejea tena kwenye serikali ya mseto imekuja baada ya Rais Omar Hhassan al Bashir kutia saini ridhaa ya kutoa nafasi katika baraza la mawaziri kwa wanachama wa kundi hilo la zamani la waasi la Sudan Peoples Liberation Movement SPLM.

SPLM ikiongozwa na makamu wake wa Rais Salva Kiir ilijitoa kwenye serikali hiyo mwezi Oktoba mwaka huu kwa kile ilichodai serikali kushindwa kutimiza yaliyomo kwenye mkataba wa amani uliyosainiwa mwaka 2005.