1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa LRA wasema hawataki vita

Mwadzaya, Thelma10 Julai 2008

Nchini Uganda kundi la waasi la Lords Resistance Army LRA limeahidi kutia saini makubaliano ya amani mwishoni mwa wiki hii kufuatia kipindi cha mazungumzo ya amani yanayokwama kila wakati

https://p.dw.com/p/EZnA
Joseph Kony Kiongozi wa waasi wa LRAPicha: AP Photo

Akizungumza na waandishi wa habari mjini nairobi kiongozi wa ujumbe wa kundi hilo David Nyekorach Matsanga amesema kuwa waasi hao hawataki tena kuendeleza mashambulizi.Kiongozi wa kundi la LRA Joseph Kony alisusia shughuli ya kutia saini makubaliano ya amani mwezi Aprili mwaka huu yaliyopangwa kufanyika eneo la Juba Kusini mwa Sudan.Joseph Kony anasakwa na Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC kwa madai ya uhalifu wa kivita na usajili wa watoto katika vita.Sikiliza taarifa ya Mwai Gikonyo aliyehudhuria mkutano huo vilevile mahojiano na Captain Chris Magezi naibu msemaji wa jeshi la Uganda.