Waasi wa LRA wasaini mkataba na serikali ya Uganda | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 24.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Waasi wa LRA wasaini mkataba na serikali ya Uganda

Mkataba wa mwisho kusainiwa katika siku chache zijazo

default

Mwanajeshi kijana wa kundi la LRA Samuel Okumu akiwa na bunduki lake katika mpaka wa Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Kundi la waasi wa Lord´s Resistance Army, LRA, limesaini mkataba wa kudumu na serikali ya Uganda wa kusitisha mapigano, katika hatua nyengine muhimu kuelekea kufikiwa kwa mkataba wa mwisho wa amani.

Pande hizo mbili zilisaini mkataba huo wakati wa mazungumzo ya amani katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba. Msemaji wa ujumbe wa serikali ya Uganda katika mazungumzo hayo, Chris Magezi, amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuumaliza mzozo wa kaskazini mwa Uganda.

Mkataba huo utaanza kutekelezwa siku moja baada ya mkataba wa mwisho kusainiwa kati ya waasi wa LRA na serikali ya Uganda. Wapatinishi katika mazungumzo ya amani ya mjini Juba wanasema wana matumaini mkataba wa mwisho utasainiwa katika siku chache zijazo.

Joseph Ochieno wa chama cha Uganda People´s Party amesema hii ni siku nzuri kwa Uganda na kwa watu wote wanaopigania amani badala ya vita.

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika mazungumzo ya mjini Juba, rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chissano, amethibitisha kwamba mkataba huo una maana kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Uganda vilivyodumu miongo miliwi vimefika mwisho.

 • Tarehe 24.02.2008
 • Mwandishi Josephat Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DCPv
 • Tarehe 24.02.2008
 • Mwandishi Josephat Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DCPv
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com