Waasi wa kundi la JEM washambulio maeneo ya Khartoum | Habari za Ulimwengu | DW | 11.05.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Waasi wa kundi la JEM washambulio maeneo ya Khartoum

-

NEW YORK

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon amelaani vikali mashambulio ya waasi wa Darfur dhidi ya maeneo ya mji mkuu wa Sudan Khartoum na kutoa mwito wa kukomeshwa kwa mapigano hayo ambayo yanafiwa huenda yakatatiza juhudi za amani katika eneo hilo.

Serikali ya Sudan ilifahamisha kwamba jeshi lake limezuia shambulio la waasi dhidi ya mji mkuu Khartoum.Waasi wa kundi la usawa na haki JEM wanadai wameuteka mji mmoja katika eneo la magharibi mwa Khartoum katika juhudi zao za kuiangusha serikali ya Sudan. Hatua hiyo ya waasi huenda ikawa ndio kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika jaribio la kuuteka mji wa Khartoum.Utawala wa khartoum umetangaza amri ya kutotoka nje mjini humo.Walioshuhudia wanasema mapigano makali yalichukua muda wa saa kadhaa lakini hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu majeruhi.Wizara ya mambo ya ndani imetoa taarifa ya kutoa mwito wa utulivu na kuwaomba wakaazi wa mji huo wabakie majumbani mwao.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com