1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa FNL watoa masharti kusitisha mapigano

24 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E5S5

Kundi la pekee lililosalia la waasi nchini Burundi la FNL Palipehutu limetangaza kusitisha mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea kwa kipindi cha zaidi ya mwezi nna kutishia kuvunjika makubaliano ya mani kati ya serikali na waasi hao.

Kundi hilo limesema liko tayari kuachana na mapigano kwa sharti kwamba serikali nayo itafuata mfano huo na kuacha matumizi ya nguvu dhidi wapiganaji wake.Aidha amesema lazima wapiganaji wa FNL wapewe chakula na wale watu walioathirika na mapigano hayo wasaidiwe. Wakati huohuo rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunzinza amefahamisha kwamba serikali yake inaamini kuwa amani na maelewano yatapatikana kati yake na kundi hilo la FNL.

Serikali ya Burundi na kundi hilo la Fnl zilitia saini makubaliano ya kukomesha mapigano mwaka 2006 mwezi septemba lakini mapigano yamekuwa yakiripotiwa nchini humo.