Waasi wa Darfur watishia kuuteka mji | Habari za Ulimwengu | DW | 21.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Waasi wa Darfur watishia kuuteka mji

KHATOUM.Waasi katika eneo lenye mzozo la Darfur wametishia kuushambulia mji mkuu wa jimbo hilo la magharibi la Darfur El-Geneina na kuwataka wafanyakazi wa mashirika ya misaada kutokwenda katika makambi ya kijeshi ya serikali.

Jeshi la Sudan halijatoa jibu juu ya tishio hilo la waasi hao wa kundi la Justice and Equality Movement JEM, ambao walidai kupata ushindi wiki zilizopita katika mapambano na majeshi ya serikali na kuwakamata mateka wanajeshi 29 wa serikali. Hata hivyo serikali ya Sudan ilikanusha.

Kiongozi wa kundi hilo Khalil Ibrahim amesema kuwa vikosi vyake vimeuzingira mji huo mkuu wa Darfur kutoka pande zote na kuwataka wafanyakazi wa misaada kutoogopa lakini wachuke tahadhari ya kubakia kwenye maeneo yao.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com