Waasi wa Chad walikataa jeshi la Umoja wa Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 11.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Waasi wa Chad walikataa jeshi la Umoja wa Ulaya

Waasi wa Chad wamezitolea mwito nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zisipeleke wanajeshi wao wa kulinda amani katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Waasi hao wanadai kikosi hicho cha kulinda amani cha Umoja wa Ulaya kitaegemea upande mmoja kwa kuwa kina idadi kubwa ya wanajeshi kutoka Ufaransa.

Muungano wa makundi ya waasi umesema Ufaransa ambayo inachangia zaidi ya nusu ya wanajeshi 3,700 wa jeshi la Umoja wa Ulaya kwa ajili ya Chad, EUFOR, ilimsaidia rais Idriss Debby kukabiliana na uvamizi wa waasi hao dhidi ya mji mkuu Ndjamena mwanzoni mwa mwezi huu.

Katika taarifa yao ya pamoja waasi wa Chad wamezitaka nchi za Umoja wa Ulaya zisipeleke majeshi yao wakiamini lengo la jeshi la EUFOR ni kuulinda utawala wa rais Deby.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com