Waasi kuendelea kupambana na serikali Congo | Habari za Ulimwengu | DW | 14.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Waasi kuendelea kupambana na serikali Congo

GOMA

Waasi wa Generali wa Kitusti Laurent Nkunda hapo jana wameapa kupambana na serikali ya Congo na waasi wa Kihutu wa Rwanda bila ya majuto wala masikitiko.

Kambasu Ngese akizungumza katika mkutano wa amani mjini Goma Jamhuri ya Kidemokrasi kama mkuu wa ujumbe wa Nkunda ameitaka serikali ya Joseph Kabila kuwatimuwa nchini Congo wapiganaji wa Kihutu wa Rwanda wanaokadiriwa kufikia 6,000 ambao amewaita kuwa kikosi cha mauaji ya kimbari.

Wanamgambo hao wanaonekana kuwa kikwazo kikuu cha kurudi kwa takriban Watutsi wa Congo 40,000 waliojitafutia hifadhi nchini Rwanda.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com