1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi wa habari na harakati za upatikanaji wa amani ulimwenguni.

Scholastica Mazula4 Juni 2008

Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya habari limemalizika leo mjini Bonn, Ujerumani.

https://p.dw.com/p/EDbH
Kunda Dixit ni mmoja wa washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Waandishi wa habari lililofanyika Bonn, kutoka Nepal.Picha: GMF

Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa katika kongamano hilo ni pamoja na ushiriki wa Vyombo vya habari ulimwenguni katika kuleta na kuimarisha Amani.

Kongamano hilo ambalo limewashirikisha waandishi kutoka sehemu mbalimbali ulimwengu, Mashirika ya Kimataifa na wadau mbalimbali, limeweza kujadili masuala kadhaa ya kiwemo mazingira magumu ya uandishi wa habari na utoaji wa habari sahihi kwa jamii.

Miongoni mwa yalijadiliwa ni pamoja na waandishi kutoa ripoti za kweli bila kupendelea upande wowote,habari zenye kusaidia kujenga umoja, Demokrasia na haki za Binadamu.

Waandishi wa habari wanajukumu la kuwafahamisha watu juu ya mizozo mbalimbali lakini kwa njia ambayo haitaleta mgangano kati ya watu.Hii ni pamoja na katika maeneo yenye vyombo vya habari vinavyorusha matangazo ya Kikabila kwa mfano Rwanda, Kenya na maeneo mengine.

Charles Otieno ni mwandishi wa habari katika Gazeti la East African Standard nchini kenya ambaye ni mmoja wa washiriki wa Kongaamano hilo, anasema kongamano hilo limemsaidia sana kutambua wajibu wake kama mwanddishi wa habari na jinsi anavyoweza kuchangia upatikanaji wa amani.

Aidha Washiriki walimeweza kujadili pia jinsi waandishi wa habari wanavyonyimwa uhuru wa kufanya kazi zao ikiwa ni pamoja na baashi ya Vyombo vya habari kufungwa kama vile, nchini Zimbabwe, na Kenya.

Hata hivyo waandishi wa habari wamepewa changamoto za kuendelea na kazi yao katika jamii lakini pia kwa moyo wa kushirikiana kwa pamoja kama familia.

Akihitimisha kongamano hilo Mkurungezi wa Deutsche Welle, Erik Bettermann, amepongeza majadiliano na maadhimio yaliyofikiwa katika Kongamano hilo ya kuwalinda waandishi wa habari katika matatizo hususani kwenye nchi zenye migogoro.

Amesema vyombo vya habari vya Kimataifa vinapaswa kusaidia kutoa taarifa bila upendeleo kwa kutoa taarifa sahihi ambazo vyombo vya habari vya Kawaida vya baadhi ya nchi haviwezi kuzitoa kulingana na masuala ya usalama.

Bettermann amefafanua kuwa yombo vya habari vinapaswa kusaidia kumaliza migogoro na kusaidia harakati za upatikanaji wa amani.

Kongamano hili la siku tatu la Vyombo vya habari liliandaliwa na Deutsche Welle na lilikuwa likijadili wajibu wa Vyombo vya habari katika kujenga amani na kuzuia migogoro.

Bettermann, amehitimisha kongamano hilo kwa kutangaza kongamano jingine kama hilo litakalofanyika mwakani mjini Bonn, ambalo litaangalia zaidi changamoto za utandawazi na jukumu la vyombo vya habari, masuala ya Kiteknolojia, matumizi ya vifaa vya kisasa na athari zake kwa Vijana.