Waandamanaji wameshambuliwa nchini Yemen | Matukio ya Kisiasa | DW | 30.05.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Waandamanaji wameshambuliwa nchini Yemen

Watu 4 wameuawa na wengine 90 wamejeruhiwa katika makabiliano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji nchini Yemen

default

Mapigano yameenea nje ya mji mkuu Sana'a

Vikosi vya usalama nchini Yemen viliwashambulia waandamanaji katika mji uliopo kusini,Taiz hapo jana na kuwaua watu 4 na kuwajeruhi wengine 90.

Jemen Demo Soldaten

Wanajeshi wa Yemen waliosaliti amri na kujiunga na waandamanaji

Maafisa katika hospitali wamesema vikosi hivyo vya usalama vinavyomuunga mkono rais Ali Abdullah Saleh, viliwashambulia kwa silaha waandamanaji.

Mapema hapo jana upinzani nchini humo na waziri wa zamani wa ulinzi aliyejiuzulu serikalini, jenerali Abdullah Ali Aleiwa, walimlaumu rais huyo kwa kuuruhusu mji uliopo kusini, Zinjibar, kuanguka mikononi mwa kundi la kigaidi la Al Qaeda, ili ayashawishi mataifa ya magharibi yamruhusu asalie madarakani.

Mwandishi:Maryam Abdalla/Afp/Rtre.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com