Waandamana Yemen kutaka nchi hiyo kumegwa katika mapande mawili | Habari za Ulimwengu | DW | 13.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Waandamana Yemen kutaka nchi hiyo kumegwa katika mapande mawili

SANAA:

Waandamanaji wanne wamejeruhiwa katika maandamano yaliyofanyika mjini Sanaa mji mkuu wa Yemen.

Maelefu ya waandamanaji jumapili walipambana na polisi ya kutuliza ghasia baada ya waadamanaji hao kutaka nchi hiyo igawanywe mara mbili.

Polisi imetumia maji pamoja na risasi za moto kuutawanya mkutano uliokuwa katika mji wa bandari wa Aden. Serikali hajasema lolote kuhusu kisa hicho.Baadhi ya wandamanaji waishio katika sehemu ya kusini ambayo zamani ilikuwa inatawaliwa kwa mfumo wa kijamaa wametaka eneo lao lijitenge kutoka la kusini ambalo liliunganishwa mwaka wa 1990 na kuwa nchi moja.

Agosti mwaka jana maelfu ya wandamanaji katika mji mkuu wa Sana waliitaka serikali ya Yemen kujiuzulu wakidai kuwa imeshindwa kuinua hali ya maisha ya mtu wa kawaida.Bei ya vitu muhimu vya kawaida imepanda kupita kiasi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com