1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamaji wavamia bunge Burkina Faso

Admin.WagnerD30 Oktoba 2014

Waandamanaji nchini Burkina Faso wamelivamia bunge la nchi hiyo baada ya purukushani na vikosi vya usalama.

https://p.dw.com/p/1DeLW
Burkina Faso Protest Ausschreitungen Parlament Brand
Picha: Getty Images/ AFP/ Issouf Sanogo

Hatua yao ni sehemu ya upinzani dhidi mpango wa kumzuwia Rais Blaise Compaore kugombea muhula mwingine katika uchaguzi mkuu, wakati bunge lilikuwa likutane leo kulijadili pendekezo.

Mpiga picha wa shirika la habari la Uingereza Reuters, anasema mkasa huo unatokea kabla ya kutekelezwa kwa hatua ya bunge la Burkina Faso kupigia kura itakayotoa ridhaa kwa kiongozi huyo kusimama katika kinyang'anyiro kijacho cha urais.

Polisi wanasemekana sasa wamejiondoa na kuwaachia waandamanaji kuingia ndani ya jengo hilo la bunge.

Kabla ya kufikia hatua hiyo polisi wa walifuata na kuwapiga baadhi ya wafuasi wa upinzani, ambao walikuwa wakijaribu kulifikia jengo la bunge mjini Ouagadugu, ambalo limewekewa uzio na jeshi la polisi. Wabunge walikuwa katika matarajio ya kupigia kura mpango uliopendekezwa na serikali, ili kuweza kufanyika mabadiliko katika katiba, iweze kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi ujao mwakani wakati huu anapomaliza muda wake.

Sauti ya upinzani

Awali upande wa upinzani nchini Burkina Faso ulitoa wito wa kuzuia hatua hiyo. Wito huo umetelewa wakati umoja wa Ulaya ukiwa tayari umekwisha sema mabadiliko ya katiba yanapaswa kuupuziliwa mbali kabisa na kuonya yanaweza kuvura amani, maendeleo na michakato ya kidemokrasia.

Gewaltsame Proteste in Ouagadougou 28.10.2014
Maandamano nchini Burkina FasoPicha: AFP/Getty Images/Issouf Sanogo

Taarifa hiyo ya Umoja wa Ulaya umezitaka pande zote mbili nchini humo kujiweka kando na vurugu.

Hapo jana benki, maduka na masoko vilifunguliwa tena baada ya kuibuka mapigano katika mitaa mbalimbali, kufuatia maandamano ya maelfu ya watu dhidi ya kile walichokiita "mapinduzi ya kikatiba" yanayofanywa na wafuasi wa rais Compaore, ambae amekuwa madarakani kwa miaka 27 sasa.

Kabla ya hali iliyojitokeza leo, mmoja kati ya maafisa kundi la wenye kutaka madiliko-Movement of People Progress-(MPP) chama chenye ushawishi mkubwa kwa vijana, Emile Pargui Pare alisema Oktoba 30, leo hii kwa Burkina Faso, ni siku wanaoiitwa "Black Spring" vuguvugu jeusi kama ilivyo kwa vuguvugu katika matiafa ya kiarabu. Akiongeza kusema limeweza kuwaondoa watawala wa muda mrefu.

Idadi kubwa ya polisi katika maeneo mengi na hasa katika mji mkuu wa taifa hilo Ouagadougou, inatokana na maandamano ya jana ambapo polisi vilevile iliwafyatulia watu hao mabamu ya machozi kuwatawanya, ambapo siku moja kabla ya tukio hilo walikiwa wakijihami kwa nondo na mawe.

Waziri wa zamani katika serikali ya Burkina Faso ambae sasa amejiunga na upinzani, Ablasse Ouedrago alisema watu watano waliuwawa katika vurugu za Jumannne.

Hata hivyo mpaka saa bado haijawa wazi, kama serikali itawaomba wabunge leo hii kuridhia mabadiliko ya kubadili muhula wa kuwepo madarakani katika katiba ili kumfanya rais Compaore awanie tena urais, au kujaribu kupitisha mabadiliko hayo kwa kutaka uungwaji mkono kutoka kwa asilimia 75 ya wabunge kama inavyohitajika kisheria.

Mwandishi: Sudi Mnette/RTR/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman