1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waalbania wakataa pendekezo la uhuru zaidi.

21 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQ2f

Brussels. Walbania wa Kosovo wamekataa pendekezo lililofanyiwa marekebisho la kuwa na kiasi kikubwa cha uhuru wa kujitawala kutoka Serbia jana, wakisisitiza kuwa hakuna mbadala katika madai yao ya jimbo hilo kuwa huru. Saa nne za mazungumzo ya upatanishi wa kimataifa ulioelezwa na pande zote mbili kuwa ya kina na yenye matatizo yalimalizika kwa pande zote kulaumiana kuhusu nani anahusika na kutopatikana muafaka. Wapatanishi kutoka umoja wa Ulaya , Russia na Marekani wanakwenda mbio ili kujaribu kupunguza mwanya baina ya pande hizo mbili kabla ya muda wa mwisho wa Desemba 10 ambapo wanatarajiwa kutoa taarifa kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa. Kosovo imetishia kutangaza uhuru iwapo hakuna makubaliano yatakayopatikana hadi ifikapo wakati huo. Viongozi wa Serbia na Waalbania wa Kosovo watakutana tena kwa duru ya mwisho ya mazungumzo katika muda wa siku tatu wiki ajayo mjini Baden nchini Austria.