1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama vya wahafidhina vyaongoza nchini Iran

15 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DOxp

TEHRAN:

Kufuatia uchaguzi wa bunge uliofanywa siku ya Ijumaa nchini Iran,matokeo yasio rasmi yaonyesha kuwa wahafidhina wenye msimamo mkali wanaongoza.Ripoti ya televisheni ya taifa inasema,vyama vinavyomuunga mkono Rais Mahmoud Ahmedinejad vimejinyakulia viti 108 katika bunge lenye viti 290 wakati wapendao mageuzi wamepata viti 33.Takriban nusu ya wapinzani wa Rais Ahmedinejad alie na msimamo mkali wa kihafidhina,walipigwa marufuku kushiriki katika uchaguzi wa hiyo jana.

Wapendao mageuzi walitumaini kunufaika kutokana na hali ya kutoridhika miongoni mwa wananchi wengi kwa sababu ya ughali wa maisha ulioongezeka kwa asilimia 19.Lakini wajumbe wengi wanaounga mkono mageuzi hawakuruhusiwa kugombea uchaguzi huo.Asilimia 64 ya Wairani milioni 44 walio na haki ya kupiga kura,walijitokeza kuchagua bunge jipya.