Vyama vya wafanyakazi vyatangaza mgomo Uturuki | Matukio ya Kisiasa | DW | 17.06.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Vyama vya wafanyakazi vyatangaza mgomo Uturuki

Vyama vya Wafanyakazi nchini Uturuki vimeanza mgomo mkubwa wenye lengo la kupinga ukandamizaji dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali, katika maandamano yalidumu kwa wiki kadhaa.

Wapinga serikali Uturuki

Türkei Istanbul Protest Gezi Park

Vyama viwili vya wafanyakazi vya Uturuki vimeanza mgomo huo wa nchi nzima kupinga vitendo vya ukandamizaji wa serikali ya taifa hilo dhidi ya waandamanaji, ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Mkuu wa Uturuki, Receip Erdogan kujitokeza hadharani na kutetea uamuzi wake wa kuwatawanya waandamanji katika bustani ya Gezi.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki, Muammer Guler amelaani mgomo huo kwa kusema sio halali na kuwaonya waandamanaji kutojitokeza mitaani. Na kwa upande wa polisi wa kutuliza ghasia leo hii pia wameripotiwa kuendelea kufyatua mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kwa lengo la kuwatawanya waandamanaji katika mitaa ya Istanbul na mji mkuu wa Ankara.

Waandamanaji watiwa mbaroni

Anti-government protesters shout slogans as they stand on barricades in Istanbul June 16, 2013. Turkish Prime Minister Tayyip Erdogan rallied hundreds of thousands of supporters at an Istanbul parade ground on Sunday as riot police fired teargas a few kilometres away in the city centre to disperse anti-government protesters. Riot police fired teargas into side streets around the central Taksim Square as he spoke, trying to prevent protesters from regrouping after hundreds were evicted from the adjoining Gezi Park, the centre of the demonstrations, late on Saturday. REUTERS/Serkan Senturk (TURKEY - Tags: POLITICS CIVIL UNREST TPX IMAGES OF THE DAY)

Waandamanaji katika bustani ya Gezi

Duru tofauti kutoka Ankara na Istanbul zinaeleza kuwa karibu watu 600 wamekamatwa katika operesheni ya polisi iliyofanywa jana peke yake.

Vyama vya wafanyakazi KESK na DSK, ambavyo vyote kwa pamoja vinawawakilisha maelfu ya wafanyakazi vimeitisha mgomo wa siku moja wenye lengo la kupinga vitendo vya polisi na kuongeza kuwa vimepanga kufanya maandamano baadae jioni.

Akizungumza na shirika la habari la AFP msemaji wa KESK, Baki Cinar amesema matakwa yao ni kwamba polisi isimamishe mara moja na kuongeza kuwa maandamano hayo yatajumisha wahandisi, madaktari na madaktari wa meno.

Kutawanywa kwa waandamanaji

Awali Jumamosi, polisi wa kutuliza ghasia nchini humo uliisafisha bustani ya Gezi, mjini Istanbul, eneo ambalo wanaharakati walikusanyika kwa takribani kwa siku 18 , mkusanyiko ambao chanzo chake kilikuwa, maandamano ya wanamazingira yaliokuwa na lengo la kupinga jitihada za serikali kukata miti katika eneo hilo la bustani na kujenga jengo la maduka makubwa ya kibiashara.

Lakini baadae maandamano hayo yakaenea nchi nzima, na Uwanja wa Taksim ukawa ndo kitovu cha maandamano. Leo polisi wa kutuliza ghasia wameendelea kuuzingira uwanja huo kwa lengo kwa lengo la kudhibiti kutokea kwa aina yeyote ya mkusanyiko. Hata hivyo jana maelfu ya waandamanaji walijaribu kukusanyika katika eneo hilo lakini polisi hao wa kutuliza ghasia waliwarudisha nyuma kwa kutumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Katika mkutano uliohudhuriwa na zaidi ya wanachama 100,000, kutoka chama chake cha Haki na Maendeleo (AKP) hapo jana, waziri mkuu wa Uturuki Receip Tayyip Erdogan alisisitiza kuwa ni wajibu wake kuamuru polisi kuwatawanya waandamanaji katika bustani ya Gezi kama onyo lake halikuzingatiwa.

Kutokana na hali hiyo ya kutumika nguvu dhidi ya maandamano ya amani Marekani na washirika wake wa nchi za magharibi, sambamba na makundi ya haki za binaadamu wamemkosoa Erdogan kwa namna anavyoushughulikia mgogoro huo.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP
Mhariri:Moahammed Abdul-Rahman

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com