Vyama vya siasa vyaungana kabla ya uchaguzi wa 2013 | Matukio ya Afrika | DW | 05.12.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Vyama vya siasa vyaungana kabla ya uchaguzi wa 2013

Nchini Kenya jana (04.12.2012) ndio iliyokuwa siku ya mwisho iliyotolewa kwa msajili wa vyama kuwasilishwa kwa makubaliano ya miungano ya kisiasa na kwa uchache miungano mitatu imeundwa kuelekea uchaguzi wa Machi 2013.

Makamo wa Rais Kalonzo Musyoka ameungana na Waziri Mkuu Raila Odinga

Makamo wa Rais Kalonzo Musyoka ameungana na Waziri Mkuu Raila Odinga

Muungano wa mwisho mwisho kuwekwa saini ulikuwa wa chama cha NVP cha Nicholas Biwott, Eugene Wamalwa wa New Ford Kenya na FPK Pack cha Cyrus Jirongo. Waziri Mkuu Raila Odinga naye ametia saini na Makamo wa Rais Kalonzo Musyoka, huku Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta na William Ruto wakiunda muungano wao pia.

Lakini sasa je miungano hii ina tofauti gani na kweli ina nia ya kushughulikia maslahi ya wananchi.? Amina Abubakar amemuuliza swali hili Cyprius Nyamwamu ambaye ni mchambuzi wa maswala ya kisiasa nchini Kenya.

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chni)

Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Mohammed Khelef

Sauti na Vidio Kuhusu Mada