1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vurugu zazuka tena bungeni Uganda

John Juma
27 Septemba 2017

Vurugu zilizuka tena kwa siku ya pili mfululizo katika bunge la Uganda kutokana na mswada tete wa kutaka kubadilisha katiba ili kuondoa kikomo cha umri wa rais ili kuurefusha utawala wa Rais Yoweri Museveni.

https://p.dw.com/p/2kooT
Uganda Kampala Parlament Debatte
Picha: Reuters/J.Akena

Vurugu zilizuka tena kwa siku ya pili mfululizo katika bunge la Uganda kutokana na mswada tete wa kutaka kubadilisha katiba ili kuondoa kikomo cha umri wa rais ili kuurefusha utawala wa Rais Yoweri Museveni. Baadhi ya wabunge wa upinzani pia walikabiliwa na kufurushwa bungeni baada ya Spika wa bunge Rebecca Kadaga kuwazuia kuhudhuria vikao vya bunge jana kwa kutojiendesha visivyo.

Tume ya mawasiliano Uganda imepiga marufuku vituo vya televisheni na radio kuonyesha au kutangaza moja kwa moja vikao vya bunge kutokana na vurugu hizo ikidai inachochea umma, matangazo ni ya kibaguzi, yanachochea uhasama, kuendeleza tamaduni ya ghasia na huenda yakasababisha ukosefu wa usalama wa umma.

Rais Museveni ambaye ameitawala Uganda tangu 1986, ana umri wa miaka 73 na katiba ilivyo sasa haimruhusu mtu aliye zaidi ya miaka 75 kuwania urais.