1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vuguvugu la upinzani nchini Urusi halina bado mpango

3 Desemba 2012

Jinsi makundi tofauti ya upande wa upinzani nchini Urusi yalivyopania kuungana,ili kupigania mageuzi ya kina ikiwa ni pamoja na uhuru wa vyombo vya habari na taifa linaloheshimu sheria

https://p.dw.com/p/16ugl
Jengo la Kreml mjini Moscow,kitovu cha madaraka nchini UrusiPicha: Fotolia/Irina Fischer

Ni kinyang'anyiro cha kuania madaraka.Nani mwenye usemi nchini Urusi?Taasisi ya uongozi,ijulikanayo kama "Silowiki:yaani jeshi,Polisi na idara ya upelelezi? Au upande wa upinzani?Ni mapambano kwa njia zisizo sawa:Upande mmoja inakutikana kambi yenye nguvu ya serikali inayoongozwa na Putin na upande wa pili linakutikana vuguvugu linalohasimiana la upande wa upinzani.Vuguvugu hilo sasa linataka kuungana na kuzungumza kwa sauti moja na ndio maana limeunda kupitia mtandao wa internet baraza la usimamizi linalopanga kuyaleta pamoja makundi yote.

Mashujaa lakini hawana msimamo mmoja

Ni makundi ya vijana ambao dhamiri yao ni moja tu:Mustakabali bila ya kuamrishwa na serikali-mustakbali "bila ya Putin".Isabelle Magkoeva ameanza kujiunga na waandamanaji tangu Decemba mwaka 2011,hivi sasa akiwa na umri wa miaka 21,yeye ndiye anaeongoza vuguvugu "Occupy Moscow".Professor huyo wa taaluma za Japan anatambua kikamilifu umuhimu wa malalamiko yao:"Tunaandaa mapinduzi".Hawakubaliani na msimamo wa wazee wao wa kutojishughulisha na siasa:Kuna vijana wa hirimu yangu ambao hawajui chochote kuhusu Umoja wa Usovieti.Kinyume na kizazi cha wazee wetu,sie hatuna woga! Na hatuna dharau,tunaamini kuna uwezekano wa kuleta mageuzi nchini mwetu."Kwa hivyo anategemea zaidi uungaji mkono wa vijana wenye umri kama wake"anasema Magkoeva.

Hawana wanachokiogopa,hivyo ndivyo walivyo waandamanaji vijana.Na mpango maalum pia hawana.Sawa na kwamba hawapiganii kitu kimoja.Upande wa upinzani ni mchanganyiko tangu wa wanaharakati wa usafi wa mazingira,makundi ya wanaopigania uchumi wa soko huru hadi kufikia wazalendo wanaofuata siasa za mrengo wa kulia.Mkuu wa kundi la wafuasi wa siasa kali za kizalendo,Dmitri Djomuschkin anapenda kujinata kwamba ana maingiliano na wapinzani mashuhuri wa serikali mfano wa naibu waziri mkuu wa zamani Boris Nemzow na mkuu wa wafuasi wa mrengo wa shoto Segej Udalozow.

Russland Politische Aktivistin Xenia Sobtschak
Mwanaharakati Xenia SobtschakPicha: DW

Ujerumani ndio mfano mwema wa vuguvugu la walinzi wa mazingira

Hata baraza la usimamizi halina msimamo mmoja.Mwanaharakati wa usafi wa mazingira Jewgenija Tschirikova ambae pia ni mwanachama wa baraza hilo alimshambulia msemaji wa baraza hilo Nawalny na kufika hadi ya kusema anabadilisha msimamo wake sawa na kinyonga.Maarifa aliyojikusanyia Jewgenija Tschirikowa barani Ulaya na nchini Ujerumani ndio chanzo cha kuamka kwake."Maarifa hayo yamenivutia,kwasababu vuguvugu kama hilo halijakuwepo nchini Urusi.Mfano nchini Ujerumani nimeona jinsi watu wanavyopania kupigania misimamo yao,wanateremka majiani wanaunda makundi ya wanaharakati.Kuanzia mashina sio kileleni."Hayo ndiyo yaliyompa moyo kujaribu kuanzisha vuguvugu kama hilo nchini Urusi.

Wengi lakini wa wananchi hawana moyo kama huo wa ujasiri:hata kama maandamano hivi sasa yamevuka mipaka ya Petersburg na Moscow na kuingia katika miji mengine-jamii ya tabaka ya kati haijajiunga na maandamano hayo.Wenye umri wa kati ya miaka 30 hadi 40 wanashughulika na kazi zao tu na kuhakikisha wanalipwa mishahara kuweza kuhudumia familia zao.Ukosefu wa wasaa na hofu wasije wakaorodheshwa katika "orodha nyeusi" ndiyo mambo yanayowazuwia wasijiunge na waandamanaji.Wengi wa jamii ya tabaka ya kati,hawataki kuitia hatarini neema ya kiuchumi waliyo nayo.

Mfano wa Anastassia Mescherjkova,mama wa watoto wawili anaewalea peke yake na kumiliki mikahawa miwili mjini Moscow ."Nnataka kitu kimoja tu:kwamba sheria za nchi yetu zitumike ipasavyo pia.Nadharia gani,mrengo wa kushoto,kulia,kiliberali au Social Democrats?Hajali anasema,wala suala hilo halimshughulishi-anataka kanuni ambazo kila mmoja ataziheshimu-yaani serikali,taasisi na wananchi.

Kama tabaka hiyo ya kati itazindukana kufuatia visa vya kukandamizwa haki za kiraia?Anastassia Mescherjakowa anahisi uwezekano upo."Miaka 10 iliyopita anasema watu walikuwa hawasubuti kuzungumzia siasa,hivi sasa mambo yamebadilika.

Serikali ya Urusi inatumia kila hila kuwazuwia watu kama Anastassia Mescherjakowa wasijiunge na waandamanaji.Wanatumia vitisho mfano kwa kuwakamata na kuchukuliwa hatua kali,wanazuwiliwa vibali vya kuitisha mikutano na kadhalika.Licha ya vizuwizi vyote hivyo upande wa upinzani umeshasema vuguvugu la maandamano litapamba moto mwezi huu wa Decemba.

Chama kipya cha upinzani kimeundwa."chama cha Muungano wa wananchi" kinapanga pia kuitisha mkutano wake wa kwanza mwezi huu.Vladimir Aschurkow,mshauri wa mwenyekiti wa chama hicho Aleksej Nawalny,ambae hadi hivi karibuni alikuwa meneja wa shirika kubwa la fedha na viwanda nchini humo anasema chama chao kimelenga kuwavutia wale wote ambao hawakubaliani na utawala wa kimabavu na wala rushwa.Wanaiangalia Urusi anasema kama nchi "ya Ulaya na wanapigania masilahi ya jamii ya tabaka ya kati."

Angalao katika mada moja makundi yote hayo,likitengwa lile la wakoministi, yana msimamo mmoja :yanapinga mtindo wa kupokea amri kutoka kwa Putin.Wanapigania uhuru zaidi na nchi yao kuelekezwa upande wa Ulaya.Wanapigania taifa linaloheshimu sheria,uhuru wa vyombo vya habari na serikali inayofaa.

Mwandishi:Schaeffer,Ute(DW Chefredaktion)/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Yusuf Saumu