1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUbelgiji

Von der Leyen kukabiliwa na kura ya imani Oktoba

16 Septemba 2025

Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, atakabiliwa na mijadala miwili ya kura ya Imani dhidi yake katika Bunge la Ulaya mwezi Oktoba.

https://p.dw.com/p/50ZxK
Ursula von der Leyen, rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya
Ursula von der Leyen, rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa UlayaPicha: Pascal Bastien/AP Photo/picture alliance

Rais wa bunge la Ulaya Robert Metsola amewaambia wabunge kwamba hoja mbili zimepata idadi inayohitajika ili kupigiwa kura ya imani.

Wiki iliyopita, makundi mawili ya kisiasa yanayoegemea marengo ya kulia na shoto, yalitangaza azma yao punde tu baada ya Von der Leyen kuwahutubia wabunge hao na kuainisha vipaumbele vyake katika miaka ijayo.

Kundi la siasa za mrengo wa kulia Patriots limekosoa sera ya kiuchumi ya halmashauri hiyo, huku Kundi la mrengo wa shoto likiituhumu halmashauri hiyo kwa uzembe kuhusu hali inavyozidi kuzorota katika Ukanda wa Gaza.

Mnamo mwezi Julai, Von der Leyen alishinda kura ya imani iliyowasilishwa dhidi yake katika bunge hilo.