Volland asaini mkataba na Leverkusen | Michezo | DW | 20.05.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Volland asaini mkataba na Leverkusen

Bayer Leverkusen imemsaini mshambuliaji Kevin Volland kutoka Hoffenheim. Volland mwenye umri wa miaka 23 anaripotiwa kununuliwa na Leverkusen kwa kiasi cha euro milioni 15

Volland ataiimarisha safu ya mashambulizi ya klabu hiyo katika Champions League msimu ujao. Mshambuliaji huyo wa kasi ambaye ameichezea mara sita timu ya taifa ya Ujerumani amefunga mabao 33 katika michuano 132 ya Bundesliga, yakimo mabao nane msimu huu, amesaini mkataba wa miaka mitani hadi 2021 baada ya kuwa katika klabu ya Hoffenheim kwa misimu minne.

Volland hajajumuishwa katika timu ya taifa itakayocheza dimba la Mataifa ya Ulaya – Euro 2016. Bayer Leverkusen walimaliza katika nafasi ya tatu katika Bundesliga msimu uliokamilika na watacheza hatua ya makundi ya Champions League.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com