Viwanjani wiki hii | Michezo | DW | 22.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Viwanjani wiki hii

Mashindano yariadha ya Ulaya yaanza leo mjini Munich.Mkurugenzi wa shirika la dunia la kupiga vita doping (WADA) azuru Ujerumani na Real madrid yatafuta kocha mpya .

Mashindano ya ubingwa wa riadha ya ulaya, yameanza mjini Munich,Ujerumani-kituo cha michezo ya olimpik 1972.

Rais wa Shirika la ulimwengu la kupiga vita madhambi ya doping-matumizi ya madawa kutunisha misuli-WADA-aamini kuwa Ujerumani ina zana za kutosha kupiga vita madhambi hayo.

FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni- yafafanua masharti ya wachezaji wa asili ya nchi nyengine kuzichezea timu za taifa za nchi walikokulia au kuzaliwa.Na Real Madrid yasaka bado kocha mpya ,je, atakuwa Bern d Schüster,mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani ?

Bado si wazi nani atachukua nafasi ya Fabio Capello kuwa kocha wa mabingwa wapya wa Spain-Real Madrid.Pia si wazi, nani atakuwa mkurugenzi wake kwavile, Pedja Mijatovic, huenda akajiuzulu baada ya kusikia kocha Capello ataondoshwa na nafasi yake kuchukuliwa na Bernd Schüster,mchezaji wa zamani wa taifa wa Ujerumani na kocha wa klabu nyengine ya Spain.

Real Madrid inampoteza pia staid wake david Beckham,anaeshikilia kujiunga na Los Angeles galaxy.Real ilitawazwa jumapili iliopita mabingwa wa Spian kwa mara ya 30 walipoipiku katika mechi ya mwisho mahasimu wao FC Barcelona.

FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni lilifafanmua wiki hii sheria zake znazowazuwia wachezaji kuzichezea timu za taifa waliko isipokuwa wamechukua uraia kamili wan chi hizo.Kutokana na ufafanuzi huo, mzaliwa wa Argentina Roberto Colautti na mzaliwa wa Nigeria toto tamuz hawataweza tena kuichezea timu ya Taifa ya Israel.Israel inajikuta katika changamoto na Croatia,Russia na Uingereza kuania nafasi ya finali za mwakani za kombe la Ulaya la mataifa huko Switzerland na Austria.

Israel ina miadi na Uingereza tayari septemba 8 uwanjani Wembley.

Uamuzi huu uliokatwa na halmashauri-tendaji ya FIFA mwezi uliopita ulianza kufanya kazi kati ya wiki hii pale wanachama wote 208 wa FIFA walipopokea barua ikiwaarifu sheria hii mpya.

Inaonesha kana kwamba,Itali mabingwa wa dunia wa dimba ni mabingwa pia wa kashfa za dimba, kwani kila kukicha kunaibuka nchini Itali kashfa mpya.

Mwaka mmoja baada ya klabu yake maarufu ya Juventus Turin kuteremshwa daraja ya pili ya Serie A-Ligi ya Itali kwa kulishia fedha kushawishi matokeo ya mechi ,kashfa mpya imeibuka wiki hii.

Mara hii inawakumba mabingwa wapya Inter Milan pamoja na mabingwa wa Ulaya AC Milan .Mshtaki wa serikali katika jiji la Milan, Carlo Nocerino, amewatuhumu viongozi wa klabu hizo 2 za Milan kuwa,zilijihakikishia leseni zao kucheza msimu wa 2005/06 kwa kupotoa hesabu za akiba zao za fedha. Adhabu huenda klabu zote 2 zikapokonywa mataji na hata kutertemshwa daraja ya pili kama ilivyofanyiwa Juventus msimu uliopita.

RIADHA:

Msimu wa riadha umepamba moto.wanariadha wa marekani wamekuwa wakijinoa nyumbani kwa mashindano yao ya ubingwa wa taifa.Wakenya walichagua mwishoni mwa wiki iliopita majogoo wao watakaowika mwezi ujao katika All-africa Games-michezo ya bara la afrika huko Algiers,Algeria na leo wanariadha wake kwa waume wa Ulaya wanaania taji la ubingwa mjini Munich.

Mabingwa watetezi uwanjani huko munich ni Ufaransa ambayo imeteremka na bingwa wao wa mita 110 kuruka viunzi Ladji Doucoure ikipania kutetea taji lao.

Doucoure alieshinda medali ya dhahabu huko Helsinki,finnland 2005 wakati wa ubingwa wa dunia ni miongoni mwa ma