Vita vyaibuka upya Syria | Magazetini | DW | 21.09.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Vita vyaibuka upya Syria

Wahariri wamejishughulisha na mada tatu.Hotuba ya rais Barack Obama katika hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa,,msimamo mpya wa Kansela Angela Merkel kuhusu suala la wakimbizi na vita vya syria

Obama akihutubia hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa kwa mara ya miwhso kama rais wa Marekani

Obama akihutubia hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa kwa mara ya miwhso kama rais wa Marekani

Westfälische Nachrichten

Mhariri wa gazeti hilo anaanza kwa kuuliza je Obama amevunjwa moyo? Aliwekewa matumaini makubwa hasa baada ya kutunukiwa tuzo ya amani ya Nobel wakati alipoingia madarakani.Lakini lipo jambo moja ambalo haliwezi kupingika.Sera ya nje ya Obama ilipitiliza na haikuwa na maamuzi ya ghafla ya kupitiliza.Na ikiwa atakayemrithi nafasi yake ni Donald Trump basi mtu anaweza kusema Obama atakumbukwa Kwa maumivu.

Hannoverschen Allgemeinen Zeitung»

Kipi kinachomfanya Kansela Merkel hivi sasa alegeze msimamo kuhusiana na sera yake ya wakimbizi na hata kukiri kufanya makosa,wakati mtazamo wa wengi kwake ulikuwa haumshughulishi?Merkel amefikia hadi kusema mbele ya camera kwamba laiti angeweza basi angerudisha wakati nyuma.Lakini msimamo huu mpya wa kiongozi huyo unaweza pengine kutuliza jazba na mijadala hata ile inayohusu suala la kuwepo ukomo wa viwango vya wakimbizi watakaoruhiswa Ujerumani linalopigiwa upatu na chama cha Christian Social Union CSU. Merkel alishawahi kusema kwamba hahitaji kusikia suala la takwimu.Kwahivyo kansela huyo halazimiki kuchukua juhudi kubwa kuwajali wanaomkosoa ikiwa hataki kugombea kurudi tena madarakani mwaka 2017.

Nordwest-Zeitung»

Kwa kipindi cha wiki moja iliyopita hakika ilikuweko nuru ya matumani kiasi.Kwakuwa makubaliano ya kusitisha vita yalifikiwa kati ya Marekani na Urusi. Lakini sasa ni wazi mpango huo wa amani ulikuwa wa muda tu kabla ya kuanzishwa tena kwa wimbi la mashambulizi,tena ya ukatili mkubwa dhidi ya msafara wa msaada wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa.Kila upande katika vita hivyo amezijaza upya zana zake za kivita tayari kuendeleza mapambano.Na kibaya zaidi ni kwamba hata nchi hizo zenye nguvu haziweki msitari katika vita hivyo.Na hata kama Barack Obama na Vladmir Putin wameonekana kweli kuwa na nia ya kulipatia ufumbuzi kwa njia ya amani suala la mgogoro huo lakini wameshindwa kutekeleza makubaliano hayo.Na kinachoonekana ni kwamba kila mshirika anapigania kwa nguvu zote maslahi yake.Kwa sababu kila mmoja anajua fika anayeshindwa katika vita hivi basi na yeye hapa ndo utakuwa mwisho wake.

Sächsische Zeitung»

Ilijionesha wazi kwamba makubaliano ya kusitisha vita yasingelidumu kwa muda mrefu kwasababu pande zote zinazohusika katika mgogoro huo ziko katika hali ya kutoaminiana kwa kiasi kikubwa.Ndo kusema kwa mara nyingine fursa ya kupatikana amani Syria imeponyoka.Laiti makubaliano hayo ya kusitisha vita yangetekelezwa kwa kipindi kirefu kidogo basi ingetoa nafasi ya diplomasia kuchukua mkondo wake na kuanzishwa tena mazungumzo ya kutafuta suluhu ya kisiasa kwa mgogoro huo.Hilo lakini haliwezekani tena na mambo yamezidi kuwa magumu.Urusi na Marekani kila mmoja anaonekana kushindwa kuwadhibiti washirika wake kwenye vita hivyo huku kila upande ukivutia kwenye msimamo wake. Ndo kusema kwahivyo janga linaendelea na pengine damu ikamwagika zaidi ya ilivyoshuhudiwa.Mamilioni ya Wasyria wanabidi kuendelea kuteseka sio tu mjini Allepo.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri:Iddi Ssessanga