1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vya kisheria juu ya uhuru wa kujieleza

Deo Kaji Makomba
21 Agosti 2020

Fainali ya ligi ya mabingwa siku ya Jumapili itashudia Bayern Munich ikikabana koo na Paris Saint-Germain. Timu hizo mbili zina mafungamano ya karibu na nchi ya Qatar

https://p.dw.com/p/3hJeA
Deutschland Symbolbild 1. FC Köln
Mashabiki wa Klabu ya soka ya Bayern MunichPicha: Imago Images/RHR-Foto/D. Ewert

Siku ya Jumatano jioni, Serge Gnabry na Robert Lewandowski waliisaidia Bayern kutinga fainali ya ligi ya mabingwa, ambapo mabingwa wa ligi ya Ufaransa, Paris Saint-Germain ndio kiunzi kinachobaki kati ya Bayern Munich na fahari ya kuwa washindi wa makombe matatu katika msimu mmoja, mara ya pili katika kipindi cha miaka minane.

Siku ile Bayern ilipoicharaza Paris Saint-Germain, shabiki mmoja wa mabingwa hao wa soka Ujerumani aliipeleka klabu hiyo mahakamani, kukata rufaa dhidi ya marufuku aliyowekewa na timu yake.

Mwezi Machi mwaka huu, shabiki huyo - mwanachama wa kikosi cha mashabiki wa Bayern anayehudhria kila mechi ya nyumbani na ugenini - alipigwa marufuku asikanyage maeneo yote ya Bayern Munich kwa muda usiojulikana, kwa kuingiza bango kinyemela katika mechi ya timu ya akiba, akipinga mechi za siku ya Jumatatu.

Dr Gerhhard Riedl anayeiwakilisha Bayern, alisema mahakamani kwamba bango hilo lilikiuka sheria za uwanjani kwa kuwa halikuwa na cheti cha usalama dhidi ya ajali ya moto, na kwamba ilikuwa mara ya pili kwa ukiukaji huo kutokea.

DFB Pokal Finale - Bayer Leverkusen vs. Bayern Munich | Tor 0 : 2
Baadhi ya wachezaji wa klabu ya Bayern wakishangilia ushindi wa goli katika mchezo wa fainali ya DFB PokalPicha: picture-alliance/dpa/J. MacDougal

Dr Andreas Hüttl, wakili anayemtetea shabiki huyo, hakukubaliana na hoja hiyo, alikiambia kipindi cha michezo cha kituo cha televisheni ya umma Sportschau, kwamba "Mwaka uliopita, zaidi ya mabango 100 yameoneshwa na hakujatolewa adhabu yoyote".

Wakili huyo alisema alichokifanya shabiki huyo wa Bayern ni uhuru wake wa kujieleza, ambao unalindwa na katibba ya Ujerumani.

''Hajamdharau yeyote, hajamtukana yeyote'', alisema wakili Dr Andreas Hüttl.

Bayern na Qatar

 Dr Hüttl anashuku kwamba Bayern inajaribu kumnyamazisha mteja wake, ambaye amekuwa akikosoa mafungamano ya udhamini wa klabu yake na Qatar, ambayo fuko lake la taifa ndilo mmiliki kamili wa Klabu ya Paris Saint-Germain.

Mwaka jana, shabiki huyo huyo alijaribu bila mafanikio, kuweka hoja katika mkutano mkuu wa Bayern Munich, kuutaka uweke kipengele katika katiba ya klabu hiyo, cha kusimami haki za binadamu.

Fußball Bundesliga Übergabe Meisterschale FC Bayern München
Mchezaji wa Bayern Munich Manuel Neuer akisherekea huku akiwa ameshika taji la ubingwa wa Bundesliga msimu uliomalizika akiwa na wachezaji wenzake. Picha: Reuters/K. Pfaffenbach

Januari mwaka huu wakati wa mazoezi ya kumi mfululizo ya Bayern Munich katika taifa hilo la Ghuba, shabiki anayekabiliwa na kesi alisaidia kuandaa hafla mjini Munich kwa jina Qatar, Haki za binadamu na FC Bayern: Mikono juu, vinywa vimefungwa?" ambapo yeye na wahamiaji wawili kutoka Nepal walizungumzia kuhusu mazingira ya kazi Qatar ambayo inajiandaa kuwa mwenyeji wa kombe la dunia la kandanda mwaka 2020.

Mwaka uliopita katika mechi za nyumbani za Bayern, kundi la mashabiki la shabiki huyo, Munich's Red Pride, mara kwa mara wameonesha mabango wakiikosoa shughuli za klabu yao na Qatar, ikiwa ni pamoja na Januri 2019 iliyowaonesha Rummenigge na rais wa klabu hiyo wakati huo, Uli Hoeness na alama za sarafu ya euro machoni mwamo wakizungumzia kuhusu mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi huku wafanyakazi watumwa wakiteseka nyuma ya pazia.

Rummenige alisisitiza wakati huo kwamba pamekuwepo maendeleo mazuri kuhusu hali ya haki za wafanyakazi wahamiaji na haki za wafanyakazi lakini wakosoaji wanaituhumu Qatar kwa kuitumia Bayern Munich kuosha au kufua taswira ya taifa la Qatar.

Chanzo:DW